` SHEIKHE SHINYANGA AWATAKA BODABODA KUACHA UHALIFU

WANDAMAN HOTEL

SHEIKHE SHINYANGA AWATAKA BODABODA KUACHA UHALIFU


Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Ismail H.Makusanya akiongoza ibada kwa waumini wa kiislam .

Na Chibura Makorongo

SHEIKHE SHINYANGA AWATAKA BODABODA KUACHA UHALIFU

Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ametoa wito kwa baadhi ya waendesha bodaboda kuacha tabia ya kukwapua mali za wananchi na badala yake kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habibu Makusanya ,ametoa wito huo leo machi,21 wakati wa ibada ya Sikukuu ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Manispaa ya Shinyanga, akisisitiza umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu na kudumisha maadili mema yaliyooneshwa katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Baadhi ya bodaboda waache mara moja tabia ya kukwapua mizigo ya wananchi barabarani, si jambo jema.Tumwogope Mwenyezi Mungu,” amesema Makusanya.

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa moyo wake wa huruma aliouonesha kwa watoto, hususan hatua ya kumlea mtoto aliyetelekezwa.

Kwa upande wake, Sheikhe wa Wilaya ya Shinyanga, Sudi Kategile, amewataka waumini wa dini zote kuendelea kuliombea Taifa pamoja na viongozi wake ili Mwenyezi Mungu awajaalie hekima na busara katika kuliongoza Taifa kwa amani na utulivu.



Baadhi ya waumini wa Kiislamu waliohudhuria ibada hiyo wameunga mkono wito wa Sheikhe Makusanya, wakisema ni muhimu kwa jamii kuzingatia maadili na sheria ili kudumisha amani na usalama
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464