` DC MASINDI ATOA ONYO KALI KULINDA VYANZO VYA MAJI NA KWANJA CHA MPIRA BUZINZA

DC MASINDI ATOA ONYO KALI KULINDA VYANZO VYA MAJI NA KWANJA CHA MPIRA BUZINZA

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026



Na Sumai Salum-Kishapu



Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi, ametoa onyo kali kwa wananchi wanaoingilia maeneo ya vyanzo vya maji na uwanja wa michezo katika Kijiji cha Buzinza, Kata ya Masanga wilayani humo.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 4, 2026 kijijini hapo, Mhe. Masindi amesema kuwa kuharibu na kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji ni kuhatarisha maisha ya wananchi na mifugo. Amesisitiza kuwa kitendo hicho kinaweza kusababisha upungufu mkubwa wa maji, vifo vya mifugo, wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta maji na hata kukumbana na wanyama wakali kama fisi.


“Mabwawa yote manne ya Kijiji pamoja na kiwanja kimoja cha mpira vinapaswa kulindwa ninaagiza Mwenyekiti wa Kijiji, Afisa Tarafa, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji na Afisa Ardhi ifikapo Ijumaa watembelee maeneo yenye migogoro na kunipatia mrejesho wa suluhu ifikapo Jumatatu Machi 9, 2026,” ameagiza Mhe. Masindi.


Pia amewataka viongozi na wazazi kuwaelimisha watoto juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira ili kulinda rasilimali za kijiji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.




Kwa upande wake, Afisa Tarafa wa Kishapu, Tano Malele, amesisitiza ufuatiliaji wa wanafunzi wanaotakiwa kuanza masomo, akielekeza kuwa ifikapo Ijumaa wanafunzi 10 wa Kidato cha Kwanza wawe wameripoti shuleni.
Afisa Tarafa ya Kishapu, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Tano Malale akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026


Naye Afisa Kilimo wa Kata ya Masanga, Ramadhani Said, amesema kata hiyo imepokea tani 221 za mbegu za pamba na viuatilifu (acrepacks) 36,022, ambapo Kijiji cha Buzinza kimepokea acrepacks 4,050. Pia wamepokea pampu 80 za kunyunyizia dawa ngavi ya Kata, huku Buzinza ikipewa pampu 10.


Amesema wakulima wameanza kuendana na kilimo cha kisasa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa mazao ya pamba, alizeti, mtama na mahindi, jambo linaloimarisha tija na kipato chao.


Katika sekta ya elimu, Afisa Elimu Kata, Peter James Daha, amesema hali ya ufaulu imeendelea kuimarika. Mwaka 2024, shule za msingi zilipata wastani wa alama 145 na kushika nafasi ya saba kiwilaya, huku mwaka 2025 zikifikia wastani wa 150 na kupanda hadi nafasi ya sita.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Madulu Kwangu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026


Ameongeza kuwa uandikishaji wa darasa la awali umefikia asilimia 99 na darasa la kwanza asilimia 98. Hata hivyo, bado kuna upungufu wa vyumba 23 vya madarasa, nyumba 34 za walimu na matundu 24 ya vyoo. Pia ameeleza changamoto ya baadhi ya wazazi kutoshiriki kikamilifu katika uchangiaji wa chakula cha wanafunzi shuleni.


Wananchi wa Masanga wamewasilisha kero mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi, ubovu wa miundombinu ya barabara,uboreshaji majengo ya Zahanati na nyumba za wauguzi, upatikanaji wa maji kupitia visima virefu katika vituo vya afya na shule, pamoja na uharakishwaji wa huduma ya umeme katika vitongoji.


Katika kuunga mkono juhudi za lishe mashuleni, Mhe. Masindi ameongoza Makutano hao kuchangisha magunia mawili ya mtama na fedha taslimu shilingi 330,000 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi katika shule ya Msingi Hilishi na Buzinza, akihimiza ushirikiano wa jamii katika kuboresha huduma za kijamii.
Mtendaji wa Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Steven Limbe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026Afisa kilomo Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Ramadhan Said akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026Afisa elimu Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Peter James Daha akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026Mtendaji wa Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Ally Mathias akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi wenye lengo la kufuatilia maendeleo ya Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga wilayani humo pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili Machi 4,2026Mkazi wa Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Justina Ngassa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo kuhusu maendeleo ya Kijiji hicho Machi 4,2026Mkazi wa Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sinze Gada akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo kuhusu maendeleo ya Kijiji hicho Machi 4,2026Mkazi wa Kijiji cha Buzinza Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Hezron Nzegere akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo kuhusu maendeleo ya Kijiji hicho Machi 4,2026






























































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464