` WACHIMBAJI MGODI WA MSASA WAJITOLEA KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI ILIYOKWAMA ZAIDI YA MIAKA 10

WACHIMBAJI MGODI WA MSASA WAJITOLEA KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI ILIYOKWAMA ZAIDI YA MIAKA 10

WACHIMBAJI wadogo wa mgodi katika kijiji cha Msasa kata ya Runzewe-Magharibi wilayani Bukombe mkoani Geita, wamejitolea kukamilisha zahanati ya kijiji hicho iliyokwama kwa zaidi ya miaka 10.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Msasa, Cosmas Ignasi ametoa taarifa hiyo mbele ya viongozi wa serikali ya kijiji waliofika kutembelea na kukagua maendeleo ya zahanati hiyo.

Ignasi amesema uongozi wa Mgodi huo umeamua kuikamilisha zahanati hiyo, kukabiliana na changamoto baada ya wakazi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika vijiji vya Katia jurani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Msasa Tulinge Paschal, amesema ujenzi wa zahanati hiyo ulianza miaka 10 iliyopita kupitia nguvu za wananchi kuanzia hatua ya msingi mpaka ujenzi wa boma, ambapo Sasa mgodi huo wa WACHIMBAJI wadogo umeamua kuwashika mkono Kwa kuamua kuamlizia ujenzi WA zahanati hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamesema, wajawazito wengi walikuwa wanashindwa kuhudhuria kliniki kutokana na huduma za afya kupatikana kata Jirani.

Wamesema zahanati hiyo itakapokamilika itapunguza adha ya kina mama, wazee na watoto kufuata huduma katika kata ya Manyovu ambayo ni umbali mrefu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464