Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Baraza la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini, limefanya kikao chake cha kikatiba kwa mwaka 2026, kikilenga kuimarisha mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji kwa viongozi wa jumuiya hiyo.
Akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Rehema Nhamanilo, aliwataka viongozi wa jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya tawi, kata hadi wilaya kuongeza umoja na mshikamano kwa kutanguliza maslahi ya wananchi mbele katika utekelezaji wa majukumu yao.
Alisisitiza kuwa madiwani wanawake wanapaswa kuondoa tofauti binafsi na kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi, akieleza kuwa siasa za makambi hazina tija katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha, aliwahimiza viongozi hao kuepuka siasa za kuchafuana na badala yake kuunganisha nguvu, kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao na kuhakikisha wanazibaini changamoto za wananchi kwa kushirikiana na halmashauri kuzitafutia ufumbuzi ili kujenga imani kwa wananchi waliowachagua.
Kwa upande wake, Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mheshimiwa Pendo Sawa, aliwakumbusha wanawake hao umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayoanza Machi Mosi na kufikia kilele chake Machi 8, 2026.
Alieleza kuwa maadhimisho ya kimkoa yatafanyika katika Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama, huku yale ya Manispaa ya Shinyanga yakitarajiwa kufanyika Machi 4, 2026 katika Shule ya Msingi Iwelyangula, Kata ya Kitangili.
Kikao hicho cha Baraza la UW,T kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo madiwani wote wanawake wilaya ya Shinyanga mjini.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Rehema Nhanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza
Kaimu Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga .Naibu Katalambula ambaye pia ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini akizungumza
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi ambaye pia ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini akifafafanua jambo kwenye kikao hichoKaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi ambaye pia ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini akifafafanua jambo kwenye kikao hicho
Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Pendo Wawa akizungumza kwenye kikao hicho


















