Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita ametoa mwezi mmoja wanafunzi wote ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wote wawe wamesharipoti shule, pamoja na wanafunzi wa darasa la awali na kwanza, ambao wamefikisha umri wa kwenda shule waandikishwe.
Ametoa maagizo hayo leo Februari 25, 2026 wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC, kilicho hudhuriwa na viongozi mbalimbalia wa serikali , chama na wabunge.
Amesema, tangu shule zifunguliwe mwezi Januari mwaka mpya wa masomo 2026, wanafunzi wa kidato cha kwanza waliripoti shule ni asilimia 79 na kusalia asilimia 21, kwa upande wa darasa la kwanza walioandikishwa kuanza shule ni asilimia 64 na 34 bado.
“Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote, hadi kufikia march 30 nataka nipate taarifa ya wanafunzi hawa ambao wamesalia kuripoti shule kidato cha kwanza, na kuandikishwa darasa la kwanza, nataka wote wawe shule,”amesema Mhita.
Afya.
Akizungumza kwa upande wa afya, amesema huduma za afya mkoani humo zimeboreshwa, pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba ya kisasa, madawa na madaktari bingwa, huku akitoa wito kwa wananchi kujinga na bima ya afya kwa wote sh.150,000 kwa familia ya watu sita.
Amesema, katika mpango huo wa bima ya afya kwa wote kwa watu wasiojiweza mkoani humo 63,541 watakatiwa bima hiyo na kupata matibabu.
Mikopo
Amesema, mkoa hu umeendelea kuwawesha vijana kupitia mikopo ya asilimia 10 mapato ya halmashauri ambapo asilimia 4 hutolewa kwa vijana na kwamba vijana wameshapatiwa sh.bilioni 1.6
Ajira.
Amesema, mkoa huo wa Shinyanga umepokea ajira mpya 562, katika sekta ya afya na elimu, na kwanza afya wamepokea watumishi wapya 251 na elimu 311.
Mazingira
Amesema katika utunzaji wa mazingira hadi sasa wameshapata miti milioni 2.3 kwa halmashauri zote za mkoa huo na zoezi hilo ni endelevu la upandaji miti.
Maji
Amesema mkoa huo umeendelee kuboresha utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, huku akiziagiza mamlaka za maji kukaa kwa pamoja na kulipana madeni, pamoja na Tanesco.
Madini.
Serikali imeendelea kuwawekea mazingira mazuri wachimbaji wadogo na hata kuwarasimisha na kuweza kukopesheka kwenye taasisi za kifedha, kupewa lessen na mitambo ya kisasa ya uchimbaji na utafiti wa madini.
Viwanda,
Amesema, wameendelea kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda, likiwamo eneo la Buzwagi Special Economic zone, Chapulwa, Nyanshimbi .
Michezo.
Amesema, mkoa huo unatarajia pia kuanzisha program ya academia ya michezo ili kukuza vipaji
Pia, amesema mkoa huo wa Shinyanga umepokea kiasi cha fedha Sh.Trilioni 1.5, fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
katika mkutano huo, ziliwasilishwa taarifa mbalimbali za sekta ya afya, elimu, uchumi, uzalishaji, mamlaka za maji, tume ya umwagiliaji, madini, Temesa, mpango wa bajeti ya mkoa kwa mwaka 206/2027 pamoja na kupitishwa mpago mkakati wa mkoa kwa mwaka 2026.2027/ 2030/2031.
TAZAMA PICHA 👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza.