
Halmashauri ya Msalala Wilayani kahama imepitisha makisio ya bajeti ya mwaka 2026/2027 ya kiasi cha shilingi bilioni 9.5 fedha ambayo ina ongezeko la shilingi milioni 800 sawa na aongezeko la asilimia 9.1
Na mwandishi wetu kutoka Msalala Wilayani Kahama.
.jpeg)
Akitoa taarifa ya makisio ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2026/2027, kaimu afisa mipango na uratibu wa halmashauri ya msalala amesema shiliongi bilioni 7.7 ni mapato halisi shilingi bilioni 1.2 ni mapato fungwa ambapo kwenye bajeti hiyo kuna ongezeko la asilimia 9.
Hata hivyo meneja wa TARURA wa Wilaya ya Kahama Eng. Masolwa Butondo amesema matengenezo na ukarabati wa barabara zimekuwa zikija kido kidogo hivyo wakala kulazimika kufanya ukarabati wa barabara taratibu taratibu kwa kuifuatia vipaumbekle vya halmashauri kwahiyo ushauri wa waheshimiwa madiwani kukarabari barabara chache na kuzikamilisha ameuchukua na ataufikisha kunakohusika.
Hata hivyo baadhi ya Wananchi wa Halmashauri hiyo ya Msalala wanasema ubovu wa barabara umeathiri shughuli zao za kiuchumi na kijamii huku wakidai kuwa magari yamekuwa yakishindwa kupita katika baadhi ya maeneo na kusababisha usafirishaji wa mazao na huduma muhimu kuwa mgumu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameiomba TARURA kufika katika maeneo hayo kufanya tathmini ya kina na kuziingiza barabara husika kwenye bajeti ya matengenezo ya dharura ili kunusuru maisha ya watu na mali zao.
Mbunge wa jimbo la Msalala Mh. Mabula Magangila ameitaka TARURA kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa pamoja na madiwani kuainisha barabara muhimu ili kuweka kipaumbele cha kutengeneza na kukarabati barabara za kipaumbele zaidi kwa wananchi.
Kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya msalala Flora Swagaswaga ameainisha kuwa changamoto ya utengenezaji na ukarabati hafifu wa barabara za halmashauri hiyo unasababishwa na maofisa wa TARURA kutohudhuria vikao vya majadiliano vya kisheria vya halmashauri na wadau hali ambayo inaendelea kukwamisha maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa halmashauri ya msalala Bi. Rose Manumba Rose Manumba amesema amejipanga kusimamia matumizi ya
bajeti hiyo iliyopitishwa ili ifanye kazi zilizokusudiwa huku akiahidi kushirikiana
na taasisi mbalimbali kama RUWASA na TARURA kuainisha miradi ya vipaumbele vya
wananch.
.jpeg)
.jpeg)


