` MCHUNGAJI BUDAGA AWATAKA VIJANA KULINDA AMANI NA KUSHIRIKI IBADA

WANDAMAN HOTEL

MCHUNGAJI BUDAGA AWATAKA VIJANA KULINDA AMANI NA KUSHIRIKI IBADA

Na Neema Sawaka ,Kahama

VIJANA  wa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa Kushiriki Katika kufanya Ibada ili kuishi maisha yatakayo mpendeza Mungu pamoja na Jamii inayowazunguka.
Hayo yamesemwa  na mchungaji   Constatine Budaga katika Ibada iliyofanika Siku ya jumapili ya kwanza ya Mwaka 2026 katika kanisa la Horeb  Internation Church lilipo Kata ya Busoka wilayani ya Kahama,

Budaga  amesema kuwa vijana wapaswa kuwa karibu na mungu hasa kwa kufanya ibada itakayo wasaidia  kuwajenga kiroho katika maisha yao pamoja na jamii inayowazunguka.

Mchungaji  Budaga amesisitiza vijana kuendelea kulinda amani ya nchi  na huku akiwataka vijana kukataa  kutumika kinyume na makusudio.

 Baadhi ya Waamini ambao  ni Vijana kutoka katika kanisa hilo Joan John  na  Zipora Musa  wamesema kuwa vijana wanapaswa kuwa mfano mzuri katika jamii na kuacha mambo ambayo yanaweza kuwaingiza katika matatizo na hivyo wanapaswa kuishi katika misingi itakayo mpendeza mungu kwani taifa lolote linategemea vijana waadilifu ili kujenga taifa bora.

mwisho.


 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464