
Tanzania inakabiliwa na vita ya kisaikolojia (Psychological Warfare) iliyoandaliwa kwa uangalifu, ikiongozwa na makundi yenye maslahi kutoka nje, hasa kutoka Ulaya, kwa lengo la kudhoofisha amani, utulivu, na kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini.
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na wimbi la taarifa za uongo na za kupotosha zikisambazwa kwa kasi na baadhi ya wanaharakati wa mitandaoni, wengi wao wakiishi kwa starehe katika nchi za Ulaya na Marekani, wakidai kuwepo kwa matukio ya kutisha kufuatia Uchaguzi Mkuu. Lengo kuu la taarifa hizi si kutoa ukweli bali ni kutia hofu wananchi, kuchafua taswira ya taifa, na hatimaye, kuichonganisha Serikali na watu wake.
EU na Matumizi ya Mbinu ya 'Shock Value'
Makundi haya ya nje yanatumia mbinu ya "Shock Value"—kusambaza simulizi za kutisha na kusikitisha—bila kuambatana na ushahidi wa kisayansi (forensic evidence), ili tu kuvutia umakini wa kimataifa, kupata 'likes', na 'views' zinazoingiza kipato au zinazotimiza matakwa ya wanaowafadhili.
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuonesha nia njema kwa kuunda Tume Huru ya Uchunguzi ya Kimahakama kushughulikia madai yoyote ya ukiukwaji wa haki, wakosoaji hawa wanapuuza chombo hicho halali. Badala ya kuwasilisha ushahidi wao kwenye Tume, wanachagua kupiga kelele Instagram na Twitter. Hii inathibitisha kuwa hawajali ukweli, bali wanachojali ni siasa za chuki na utekelezaji wa ajenda za mataifa ya kibeberu.
Hujuma ya Uchumi Kwenye Kivuli cha Haki
Swali la msingi la kujiuliza ni: Kwanini hujuma hii inatokea sasa?Jibu ni dhahiri: Huu ni uhujumu wa uchumi (economic sabotage). Wanaharakati hawa wanajua fika kuwa Tanzania iko katika kipindi muhimu cha mpito wa kiuchumi. Miradi mikubwa ya kimkakati kama Reli ya Kisasa (SGR) na Bwawa la Nyerere inakaribia kulipa na kuweka msingi imara wa maendeleo.
Njia pekee ya mataifa ya Magharibi na wa-proxy wao kukwamisha juhudi hizi ni kwa kutengeneza taswira ya "Taifa Lisilo Salama" ili:Kufukuza wawekezaji wa kimataifa wanaotaka kushiriki katika uchumi wetu.Kutisha watalii ambao ndio chanzo kikuu cha mapato ya kigeni.
Hili ni pigo la moja kwa moja kwa jitihada za Rais Samia za kuendeleza ajenda ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, Reconstruction), ambayo ndiyo njia ya kistaarabu ya kutatua changamoto zetu bila machafuko.
Ulinzi wa Taifa na Wajibu wa Raia
Watanzania tunapaswa kuwa macho na kukataa kutumiwa kama daraja la wanasiasa waliofeli au wanaharakati wanaolipwa na mabeberu kuleta machafuko.Tusiamini taarifa za mitandaoni zinazoashiria vurugu, hasa kutoka kwa majina au akaunti bandia.
Tuunge Mkono juhudi za uongozi wa Rais Samia, ambao umedhihirisha kuwa sikivu na unaofuata sheria.
Kama inavyosisitizwa na wananchi: "Vijana tuendelee kuwa nguzo ya amani—tulinde taifa letu." Taswira ya Taifa letu Inazidi kuwa imara hata kama mtaharibu kwa kulipwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464