` JMAT:HOTUBA YA RAIS SAMIA IMEPONYA MIOYO YA WATU ILIYOKUWA NA MAJERAHA

JMAT:HOTUBA YA RAIS SAMIA IMEPONYA MIOYO YA WATU ILIYOKUWA NA MAJERAHA



Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT)Mkoa wa Shinyanga,imepongeza Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan,wakati akihutubia Bunge, kuwa imeonyesha dira ya Taifa pamoja na kuponya mioyo ya watu iliyokuwa na majeraha.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Balilusa Khamis,akiwa na wajumbe wake,wamebainisha hayo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari.
Amesema,wanampongeza Rais Samia kwa kuendelea kuliongoza vyema taifa pamoja na kuhakikisha Amani na utulivu inaendelea kutawala hapa nchini, huku wakisifia hotuba ambayo aliitoa wakati akifungua Bunge Jijini Dodoma kuwa, imeonyesha dira ya Taifa.

"Tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa hotuba yake nzuri ambayo aliitoa Bungeni ili wafariji na kuponya mioyo ya watu iliyokuwa na majeraha na kuonyesha muelekeo wa dira ya taifa letu,"amesema Sheikh Balilusa.

Amepongeza pia Rais Samia, kwa kuunda Wizara mpya ya vijana, ambayo itatua changamoto nyingi ambazo huwakabili vijana, huku akimuomba aendelee kusimamia maridhiano.

Aidha,amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, kwa kuendelea kusimamia Amani ya Mkoa huo na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi kama kawaida.

Naye,Katibu wa Baraza la Ushirikiano wa Dini Mbalimbali Mkoa wa Shinyanga Askofu Jacob Salu, amewataka Watanzania kudumisha Amani ya nchi na wasikubali kutumika kuivuruga.

TAZAMA PICHA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT)Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akizungumza.
Katibu wa Baraza la Ushirikiano wa Dini Mbalimbali Mkoa wa Shinyanga Askofu Jacob Salu,akizungumza.
Mjumbe wa JMAT Moshi Ndugulile akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464