ππNa mwandishi wetu kutoka Mkoani Shinyanga.ππ

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka katika mikoa mbali mbali Nchini wamezindua kikundi chao kinachojulikana kwa jina wachimbaji group chenye lengo la kuhakikisa wachimbaji wadogo wanaondokana na changamoto ya kukosa mitaji ya kununua vifaa vya kisasa vya uchimbaji wenye tija.

Akisoma risala wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na harabee ya kutafuta fedha za kujenga mtambo wakisasa wa kuchenjua dhahabu (CIP), katibu wa kikundi Bw. Japhet Maligobwiru amesema kikundi hicho kilianzishwa mwezi May 2025 kikiwa na wanachama saba tu na hadi kinazinduliwa tarehe 19 Octoba 2025 kikundi kina wanachama takriban 78.

Pia amesema kikundi kimefanikiwa kukuza mtaji kutoka shilingi 3,500,000 ya awali na kufikia shilingi 58,000,000 katika kipindi cha miezi mitatu ambapo haramee inatafuta kiasi cha shilingi milionio 350 na kikundi kiwezeshe shilingi milioni 300 kupitia vyanzo vyake vya mapato ili kununua mtambo huo wa shilingi milioni 600,500,000
Aidha katibu wa kikundi amezitaja changamoto zinazokikabili kikuni kuwa ni pamija na ukosefu wa mitaji ya kuweza kuwekeza kwenye shughuli za uchimbaji na kupata vifaa vya kisasa vyenye tija, migogoro mbalimbali pamoja na elimu duni kuhusu masuala ya fedha.
Afisa mikopo na uhusiano wa benki ya NMB wilaya ya kahama Bi. Beatrice Mariki amewahakikishia wachimbaji hao wadogo kuwa benki ya nmb mikopo ya vifaa vya uchimbaji wa madini pamoja na mikiopo ya fedha taslim ambayo wanaitoa ili mkuwawezesha wachimbaji kujiendeleza kwa kununua vifaa vya kisasa na kufanya uchimbaji wenye tija.

Kwa upande wake mwe
yekiti wa kikundi hicho cha wachimbaji group bw. Juma Patrick sarungi maarufu
J. kubwa amesema malengo ya kikundui ni kuwainua wachimbaji wadogo na
kusaidiana kwenye shida na raha huku akiaiomba taasisi za fedha ziwafikie
wachimbajiu kutoa elimu ya mikopo ili wawez kukopesheka huku akiwaomba
wachimbaji wengine kujiunga na kikundi hicho ili waweze kulijenga taifa kwa
pamoja.
Kuhusu upatikanaji wa mikopo ya uhakika kwa wachimbaji wadogo, mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya kahama ambaye ni mjumbe wa chama cha wachimbaji wadogo tanzania (FEMATA) bw. Misana Nyabange ameshauri wanakikundi hao kuunganisha nguvu ya pamoja kujenga uchumi wa taifa na pia kuzitumia leseni zao za uchimbaji kukopa fedha benki.
Uzinduzi umefanyika katika Ukumbi wa MALEX ulioko Mjini Kakama tarehe 19 Octoba. 2025

