` JUMUIYA YA WAZAZI ZA CCM SHINYANGA YAOMBA KURA: JUMBE AAHIDI MAZITO KATA YA KAMBARAGE

JUMUIYA YA WAZAZI ZA CCM SHINYANGA YAOMBA KURA: JUMBE AAHIDI MAZITO KATA YA KAMBARAGE


Suzy Butondo, Shinyangablog
 Mjumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Shinyanga mjini ambaye pia  ni  mjumbe wa kamati ya utekalezaji jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Eng. James Jumbe anaendelea kuwaomba kura wananchi wa kata ya Kambarage  Mwawaza   na Kizumbi wakichague  Chama cha mapinduzi CCM ili kiendelee kuwaletea maendeleo.

 Mjumbe huyo akiwa ameambatana na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko, katibu wa Jumuiya hiyo Doris Kibabi na wajumbe wa kamati ya utekelezaji leo wamefanya ziara ya kutembelea kata ya Kizumbi Mwawaza na Kambarage kwa ajili ya kuwaombea kura wagombea wa CCM.

"leo tumekuja katika kata ya Kambarage kwa ajili ya kuwaombea kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Samia Suluhu Hassan, mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi na diwani wetu Hamis Haji ambaye ndiye tunategemea atuletee maendeleo katika kata yetu hii, hivyo niwaombe wanaccm wenzangu na wananchi wote tumchague Khamis haji ili aweze kututumikia, kwani anastahili kuwa kiongozi"amesema Eng.Jumbe.

"Naomba nisisitize kwa hapa Kambarage ambapo ndiyo nyumbani kwetu na ndipo ninapoishi nitashirikiana nae, hivyo mpeni kura na mimi nikiwa mjumbe wa kamati ya siasa tutasaidizana nae katika kuwaletea maendeleo, naomba nijikomiti kwamba akishindwa kutekeleza mimi nipo nitasimama nae bega kwa bega,ili kuhakikisha Kambarage inasonga mbele.,"amesema Jumbe.

Amesema anataka kata ya Kambarage iwe ni kata ya mfano,hivyo amewaomba kila mmoja aandae kadi ya kupigia kura ili tarehe 29 kila mmoja akapige kura katika kituo alichokaribu nacho,tukawaunge mkono wagombea wetu.

Eng Jumbe akiwa katika kata za Mwawaza amewaomba wananchi wote wamchague diwani wa kata hiyo ili aweze kushirikiana na mbunge katika kufanya kazi za kimaendeleo na kuendeleza pale alipoishia diwani aliyestaafu.

Sheila Mshandete ambaye alikuwa diwani viti maalum Shinyanga mjini amewataka wananchi wampe kura zote Khamis Haji kwa kuwa anatosha kuwatumikia wananchi wa Kambarage, pia amemuombea kura mgombea ubunge Patrobas Katambi na Rais Samia kwani ni mchapa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko amewaomba wananchi wote wajitokeze kupiga kura, tarehe 29 wakiamka tu waende kwenye vituo vya kupigia kura na wakakipigie chama cha mapinduzi CCM.

"Kuna jambo la kihuni linazungumzwa zungumzwa eti kuna maandamano, mama yetu mama Samia alizungumza mwenyewe akasema hakuma maandamano, hivyo tunatakiwa tuwahi asubuhi tukatiki kwa CCM, turudi nyumbani tusubiri tu kutangaziwa hakuna cha vurugu kutakuwa na amani tu "amesema Mrindoko.

Aidha aliyekuwa katibu wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga  mjini Ally Majeshi amewaomba wananchi wa kata ya Kambarage kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi CCM  waweze kushirikiana kufanya maendeleo, ili CCM iweze kushika dola.

"Chama cha mapinduzi CCM ndiyo chama pekee kitakachotuletea maendeleo katika kata hii ya Kambarage , hivyo niwaombe tarehe 29 tukapigie CCM ili kiweze kushika dola, kwani kimefanya maendeleo makubwa,pia ni chama kikubwa cha kwanza ambacho kinajipambanua kuisimamia na kuilinda nchi ya Tanzania  na kina historia kilipotoka na kinakoenda, hivyo tupambane ili kuhakikisha viongozi wetu wanapata kura za ushindi "amesema Majeshi

Nae mgombea wa udiwani kata ya Kambarage Khamis Haji amewaomba wananchi waendelee kukiamini chama cha mapinduzi, kwani kinaenda kutekeleza Ilani ya CCM ambayo imesheheni mafanikio, na atashirikiana na viongozi wenzake katika kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwaa kwa wakati 

Mgombea wa udiwani kata ya Mwamalili Edwin amewaomba wananchi kumchagua kiongozi anaeyeleta maendeleo si wa kuleta maandamano,amewaomba washirikiane kwa sababu ana ndoto za kuipelekea maendeleo kata ya Mwawaza
 


































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464