` GABRIEL MASANJA KUMUUNGA MKONO PATROBAS KATAMBI ASHINDE UBUNGE KWA KISHINDO JIMBO LA SHINYANGA MJINI UCHAGUZI MKUU 2025

GABRIEL MASANJA KUMUUNGA MKONO PATROBAS KATAMBI ASHINDE UBUNGE KWA KISHINDO JIMBO LA SHINYANGA MJINI UCHAGUZI MKUU 2025

Aliyekuwa Mtiania wa Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gabriel Masanja,amempongeza Patrobas Katambi, kwa kuteuliwa na Halmashauri ya CCM kupitishwa kugombea Ubunge katika uchaguzi Mkuu 2025 kupitia Chama hicho, na kuahidi kumuunga Mkono, ili ashinde kwenye uchaguzi huo, pamoja na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Madiwani wote wa CCM.

Aidha,Majina yaliyotangazwa leo Agosti 23 na Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Amosi Makalla,kuwa katika Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Paschal Katambi ndiye atapeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi CCM kugombea Ubunge katika Jimbo hilo.
Gabriel Masanja.
Patrobas Paschal Katambi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464