` TAMASHA KUBWA LA KIROHO LA TWEN'ZETU KWA YESU 2025 KUTIKISA SHINYANGA

TAMASHA KUBWA LA KIROHO LA TWEN'ZETU KWA YESU 2025 KUTIKISA SHINYANGA

TAMASHA KUBWA LA KIROHO LA TWENZETU KWA YESU 2025 KUTIKISA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TAMASHA kubwa la kiroho la Twenzetu kwa Yesu 2025 linatarajiwa kufanyika Agosti 16 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, likishirikisha kwaya mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa.
Tamasha hilo ambalo ni msimu wa pili tangu kuanzishwa kwake, limeandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, kwa kushirikiana na Upendo TV, likidhaminiwa na Jambo FM.

Mratibu Ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Mchungaji Odolous Gyunda, akizungumza leo Julai 25,2025 na Waandishi wa habari,amesema Tamasha la mwaka huu litakuwa la kipekee kutokana na Idadi nyingi ya Kwaya zitakazoshiriki na maandalizi kabambe yaliyofanyika.
“Tunakusudia kuleta kwaya zaidi ya 18 kutoka makanisa ya KKKT pamoja na kwaya kutoka madhehebu mengine, zikiwemo Neema Gasper, Agape, AICT-Kambarage, Malaika Wakuu kutoka Kanisa Katoliki na nyinginezo nyingi. Kila uimbaji utafanyika mubashara (live),” amesema Mchungaji Gyunda.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini tamasha hilo ili kuuwezesha ujumbe wa Neno la Mungu kuwafikia watu wengi kwa mafanikio makubwa.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo,Happiness Joram Gefi,alisema tamasha hilo limebeba malengo ya kuwaunganisha vijana na jamii kwa ujumla kupitia nyimbo za Injili na maombi ya pamoja.
“Ni jukwaa la kiroho kwa vijana na watu wote tunawaalika kutoka mikoa jirani kama Simiyu, Geita na Mwanza kujitokeza kwa wingi,” amesema Happines.

Aidha,ametaja bei za tiketi kushiriki Tamasha hilo kuwa ni Sh.5,000, pamoja na bei ya Tshet sh.2,0000 na kwamba zinapatikana katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga Kahama na Bariadi mkoani Simiyu.

Mdhamini wa Tamasha hilo kutoka Jambo FM,Renatus Kiluvia ambaye ni msimamizi wa vipindi vya Jambo Media,amesema Tamasha hilo litafana na kuwa sehemu ya maisha ya wananchi wa Shinyanga na Simiyu.

Kauli Mbiu ya Tamasha hilo inasema”Twenzetu kwa Yesu 2025 Ishi kwa Malengo, huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.

TAZAMA PICHA👇👇
Mratibu Ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa Kanisa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza.
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Happiness Joram Gefi akizungumza.
Mchungaji Nzinyangwa Mkiramwani kutoka KKKT ambaye ni Mratibu wa Tamasha hilo akizungumza.
Mdhamini wa Tamasha hilo kutoka Jambo FM,Renatus Kiluvia ambaye ni msimamizi wa vipindi vya Jambo Media,akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464