Kampuni ya CRJE (East Africa) Limited imeungana na mataifa mbalimbali jijini Dar es Salaam kusheherekea Tamasha la Utamaduni la watu wa China la Dragon Boat ambalo ni mahususi kwa kudumisha utamaduni.
Tamasha la Dragon Boat, pia linajulikana kama Tamasha la Duanwu, kwa kawaida huangukia siku ya tano ya mwezi wa tano katika kalenda ya mwandamo ya Kichina. Ambapo Iliadhimishwa mwaka huu siku ya jumamosi Mei 31 jijini Dar es Salaam.
Wakati wa tamasha hilo lililofanyika eneo la Masaki jijini Dar es Salaam, watu kutoka mataifa mbali mbali walifurahia tamaduni mbali mbali za watu kutoka China kama vile kula Zongzi (wali unaonata) ili kumkumbuka Qu Yuan, mshairi na mwanasiasa wa Kichina aliyeheshimika wa kipindi cha miaka ya 475 B.C.-221 B.K.
Akizungumza katika tamasha la kwanza, lililoandaliwa na CRJE (East Africa) Ltd jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa CRJE Jiang Yuntao alisema kuwa tukio hilo pia lililenga kukuza mabadilishano ya kitamaduni na maelewano kati ya China na Tanzania.
"Kama unavyoona tukio hili limevutia idadi kubwa ya Watanzania na marafiki wa kigeni, waliokusanyika ili kujionea maudhui ya kipekee ya Tamasha hilo," alisema.
"Tamasha hili pia linajulikana kama "Tamasha la Duanwu", ni moja ya sikukuu zetu kuu nne za jadi, na historia ya zaidi ya miaka 2000. Ilianzishwa ili kumkumbuka mshairi mzalendo Qu Yuan kutoka kipindi cha Vita vya Uchina. Katika siku ya tano ya mwezi wa tano katika kalenda ya mwandamo kila mwaka, Wachina husherehekea kwa kutengeneza na kula zongzi, kuvalia dragoni wa kutundika racing majani ya mugwort, ambayo yote yanaaminika kuleta afya njema, kuepusha maovu, na kuzuia magonjwa,” alisema.
Aliongeza: "Mwaka wa 2009, Tamasha la Mashua ya Joka lilijumuishwa katika orodha ya UNESCO ya Turathi za Utamaduni Zisizogusika za Binadamu, na kuwa muhimu kwa ulimwengu kujifunza kuhusu utamaduni wa Kichina."
Hata hivyo, raia wengine waliohudhuria tamasha hilo jijini Dar es Salaam walisifu tamasha hilo wakisema kuwa limeweza kuwafundisha mambo mbali mbali kuhusu utamaduni na mila za wachina.
Mtanzania John William alimwambia mwandishi wa habari kwenye tamasha hilo: “Tunashukuru kwa kupata fursa ya kujifunza tamaduni kutoka nchini China ambapo imekuwa vile vile fursa kubwa kwa mataifa mbali mbali ikiwepo Tanzania kuweza kujifunza mila na tamaduni mbali mbali.”
Aliongezea kuwa ingawa hii ni mara ya kwanza kwa tamasha hili kufanyika nchini Tanzania ana Imani kuwa likifanyika kwa mara ya pili litakuwa bora zaidi ya ilivyofanyika kwa awamu hii.