Suzy Butondo Shinyanga
Askofu wa kanisa la The Evangelist Assemblies of Church Tanzania (EAGT) jimbo la Shinyanga Michael Ernest Ngule amewataka vijana (CGM) kujihadhali na utandawazi wa simu janja ambao unaweza kusababisha kuporomoka kwa maadili.
Licha ya kuwataka wajiepushe na utandawazi wa simu janja pia amewataka kwenda kwenye jamii kubadilisha watu wamrudie Mungu ili warudi kwenye maadili mema.
Hayo ameyasema wakati akifungua rasmi kongamano la vijana (CGM) jimbo la Shinyanga ambalo linaendelea kufanyika katika kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga mjini, ambapo amewataka vijana hao kujihadhari na simu janja ili kulinda imani waliyonayo na kulinda maadili mema.
Ngule amesema kuna kilio kikubwa katika Taifa cha kuporomoka kwa maadili,kwani kuna baadhi ya vijana wamekubaliana na matangazo yanayowekwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo yamekuwa yakiharibu maadili na kusababisha kushuka kiroho.
"Tuna kilio kikubwa sana katika Taifa letu la Tanzania la kuporomoka kwa maadili,na hii inatokana na utandawazi baada ya kuanzishwa mitandao ya kijamii, vijana wengi wamebadilika na wemeshuka kiroho na kuacha kuomba na kusoma neno la Mungu, wamekuwa wakishinda wakiperuzi Twiter,facebook,whatsap na mitandao mingine,"amesema Askofu Ngule.
"Niwaombe vijana wa EAGT lazima muone mbele muwe na dira ya kukomboa muda wenu, msikubali kubadilishwa na simu janja, kuweni na elimu ya kutosha ya duniani ya kuweza kijilinda na elimu ya kiroho,ili kulinda imani yetu tunatakiwa tujifunze mwenendo wa Yesu kristo, kataeni kukamatwa na dunia bila kuwa na maadili mema Taifa letu haliwezi kuendelea "ameongeza.
Ngule amesema baadhi ya waanzilishi wa mitandao ya kijamii wametajwa kuwa ni wapinzani wakubwa wa Mungu ambao wanadai hakuna Mungu duniani, hivyo ni kujihadhari mitandao hiyo ili kuepuka kuvuviwa kipepo na kunyongwa kiroho, kwani hawapendi watu wakue kiroho, badala yake wakeshe wakiperuzi mitandao hiyo.
"Simu janja imekuwa ikiwateka watu wengi ufahamu wao, hiyo ni nguvu ya ushawishi,ambayo watu wengi wameingia na walikuwa waombaji wazuri wameacha kuomba, na kusoma neno la Mungu wapo bize na mitandao hivyo niwaombe vijana mtumie muda kwa kumtumikia Mungu wenu, kuna kazi nyingi za kumtumikia Mungu,amesema Ngule.
"Leo mmepata elimu hii, katika kipindi hiki kifupi, niwatake mkaitumie kuelimisha jamii, ili tuwe na kanisa zuri mshibe sana mambo ya kiroho akikupotosha mtu mwambie imeandikwa ni lazima usimamie imani yako ya kimungu"ameongeza.
Nae mmoja wa wawezeshaji wa Kongamano hilo Baraka Masembo kutoka Kahama amewataka vijana kuikimbia zinaa na kujilinda wenyewe ili yule muovu shetani asiwaguse, hivyo wajilinde wenyewe wasiwe la kuangusha wengine,ambapo pia aliwataka vijana wa wasivae mavazi yanayoleta vishawishi na wajiepushe na mazungumzo mabaya.
" Pia niwaombe mjitenge na dhambi kwani dhambi imesababisha vijana wengi kuwa mateja kuwa mashoga, dhambi inaharibu afya ya vijana afya ya kanisa, na inamfanya mtu azeeke kabla ya muda wake hivyo"amesema Baraka.
Mchungaji Jonas Masembo kutoka Ukenyenge amesema wao kama vijana wana changamoto nyingi sana katika maisha, kwani kutokana na utandawazi kuna vijana wengi wanaharibikiwa akili maamzi ni mabaya, na wengi wanaharibikiwa, hivyo niwasihi tumrudie Mungu na kumsikiliza maelekezo yake, pia toka tumekuja hapa tumepata madini mengi ya kiroho hivyo tutayapeleka huko kwenye maeneo yetu tukaielimishe jamii yetu iweze kumjua Mungu na kusimama katika maadili mema.
Mchungaji Goodluck Daud wa kanisa la EAGT Songambele Kitangili, ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya Class Gosple Messangers (CGM) ambao ni wajumbe wa injili wa Yesu kristo jimbo la Shinyanga, lengo la kusanyiko hilo ni jinsi gani vijana wajue kujitegemee na kumwishia Mungu, kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanakaa na jamii ambayo imechanganyika na dunia, hivyo tunawafundisha ni jinsi gani kijana ataepukana na dhambi zinazomhusu kijana.
" Vijana wengi wameporomoka katika maadili ya kijamii nawashauri wazingatie elimu ya Mungu inayotolewa kwani hakuna sayansi ama njia inayoweza kumrudisha kwa Mungu, lakini kwenye elimu ya Mungu ndipo kijana anaweza akarudishwa kwenye misingi ya imani inayoendana na jamii katika ulimwengu huu, ninawashauri wamjue Mungu ili wapate amani na watimize malengo yao hapa duniani, amesema Daud.
Baadhi ya vijana waliopata mafunzo hayo akiwemo Rehema Varelian Kuziwa amesema yeye kama kijana amejifunza somo la ikimbie zinaa, ambayo ni dhambi inatendeka ndani ya mwili, maana biblia inasema "tusiliharibu hekalu la Mungu, pia tumejifunza elimu ni ya msingi kwani inafungua fahamu na kuwa na maarifa mbalimbali, niwasihi vijana wazidi kutafuta maarifa katika kusoma vitabu mbalimbali.
Kongamano hilo lilianza june 23, /6/2025 linatarajiwa kufungwa june 27 mwaka huu, ambapo mpaka sasa ni zaidi ya vijana 500 wamekusanyika kwenye kongamano hilo kwa ajili ya kupata elimu ya kiroho,na lengo la kongamano hilo ni jinsi gani vijana wajue kujitegemee na kumwishia Mungu, kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanakaa na jamii ambayo imechanganyika na dunia, ni jinsi gani kijana ataepukana na dhambi zinazomhusu kijana na kuelimisha jamii
Askofu wa jimbo la Shinyanga Michael Ernest Ngule akionyesha kitabu cha kufundishia vijana kwenye kongamano hilo
Askofu wa jimbo la Shinyanga Michael Ernest Ngule akizungumza na vijana wa jimbo la Shinyanga
Makamu Askofu Emanuel Dubinza akizungumza na vijana wa CGM katika kongamano hilo ambapo aliwataka mafundishi watakayoyapata wakayafundishe kwenye jamii wanayoishi

Katbu wa jimbo la Shinyanga Jonas Samayytu akizungumza na vijana wa CGM kwenye kongamano hilo

Mchungaji Goodluck Daud wa kanisa la EAGT Songambele Kitangili, ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya (CGM) ambao ni wajumbe wa injili wa Yesu kristo jimbo la Shinyanga
Wachungaji wakimikiliza askofu wa jimbo la Shinyanga akizungumza na vijana wa CGM

Vijana CGM jimbo la Shinyanga wakimsikiliza Askofu akiwafundisha jinsi ya kuishi maisha ya kristo, na kuwa na maadili mema
Wachungaji wa kanisa la EAGT kutoka sehemu mbalimbali jimbo la Shinyanga
Vijana CGM jimbo la Shinyanga wakimsikiliza Askofu akiwafundisha jinsi ya kuishi maisha ya kristo, na kuwa na maadili mema
Vijana CGM jimbo la Shinyanga wakionyesha vutendea kazi walivyokuja navyo kwa ajili ya kuabdika yale watakayofundishwa
Vijana CGM jimbo la Shinyanga wakionyesha vutendea kazi walivyokuja navyo kwa ajili ya kuabdika yale watakayofundishwa

Askofu wa kanisa la The Evangelist Assemblies of Church Tanzania (EAGT) jimbo la Shinyanga Michael Ernest Ngule amewataka vijana (CGM) kujihadhali na utandawazi wa simu janja ambao unaweza kusababisha kuporomoka kwa maadili.
Licha ya kuwataka wajiepushe na utandawazi wa simu janja pia amewataka kwenda kwenye jamii kubadilisha watu wamrudie Mungu ili warudi kwenye maadili mema.
Hayo ameyasema wakati akifungua rasmi kongamano la vijana (CGM) jimbo la Shinyanga ambalo linaendelea kufanyika katika kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga mjini, ambapo amewataka vijana hao kujihadhari na simu janja ili kulinda imani waliyonayo na kulinda maadili mema.
Ngule amesema kuna kilio kikubwa katika Taifa cha kuporomoka kwa maadili,kwani kuna baadhi ya vijana wamekubaliana na matangazo yanayowekwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo yamekuwa yakiharibu maadili na kusababisha kushuka kiroho.
"Tuna kilio kikubwa sana katika Taifa letu la Tanzania la kuporomoka kwa maadili,na hii inatokana na utandawazi baada ya kuanzishwa mitandao ya kijamii, vijana wengi wamebadilika na wemeshuka kiroho na kuacha kuomba na kusoma neno la Mungu, wamekuwa wakishinda wakiperuzi Twiter,facebook,whatsap na mitandao mingine,"amesema Askofu Ngule.
"Niwaombe vijana wa EAGT lazima muone mbele muwe na dira ya kukomboa muda wenu, msikubali kubadilishwa na simu janja, kuweni na elimu ya kutosha ya duniani ya kuweza kijilinda na elimu ya kiroho,ili kulinda imani yetu tunatakiwa tujifunze mwenendo wa Yesu kristo, kataeni kukamatwa na dunia bila kuwa na maadili mema Taifa letu haliwezi kuendelea "ameongeza.
Ngule amesema baadhi ya waanzilishi wa mitandao ya kijamii wametajwa kuwa ni wapinzani wakubwa wa Mungu ambao wanadai hakuna Mungu duniani, hivyo ni kujihadhari mitandao hiyo ili kuepuka kuvuviwa kipepo na kunyongwa kiroho, kwani hawapendi watu wakue kiroho, badala yake wakeshe wakiperuzi mitandao hiyo.
"Simu janja imekuwa ikiwateka watu wengi ufahamu wao, hiyo ni nguvu ya ushawishi,ambayo watu wengi wameingia na walikuwa waombaji wazuri wameacha kuomba, na kusoma neno la Mungu wapo bize na mitandao hivyo niwaombe vijana mtumie muda kwa kumtumikia Mungu wenu, kuna kazi nyingi za kumtumikia Mungu,amesema Ngule.
"Leo mmepata elimu hii, katika kipindi hiki kifupi, niwatake mkaitumie kuelimisha jamii, ili tuwe na kanisa zuri mshibe sana mambo ya kiroho akikupotosha mtu mwambie imeandikwa ni lazima usimamie imani yako ya kimungu"ameongeza.
Nae mmoja wa wawezeshaji wa Kongamano hilo Baraka Masembo kutoka Kahama amewataka vijana kuikimbia zinaa na kujilinda wenyewe ili yule muovu shetani asiwaguse, hivyo wajilinde wenyewe wasiwe la kuangusha wengine,ambapo pia aliwataka vijana wa wasivae mavazi yanayoleta vishawishi na wajiepushe na mazungumzo mabaya.
" Pia niwaombe mjitenge na dhambi kwani dhambi imesababisha vijana wengi kuwa mateja kuwa mashoga, dhambi inaharibu afya ya vijana afya ya kanisa, na inamfanya mtu azeeke kabla ya muda wake hivyo"amesema Baraka.
Mchungaji Jonas Masembo kutoka Ukenyenge amesema wao kama vijana wana changamoto nyingi sana katika maisha, kwani kutokana na utandawazi kuna vijana wengi wanaharibikiwa akili maamzi ni mabaya, na wengi wanaharibikiwa, hivyo niwasihi tumrudie Mungu na kumsikiliza maelekezo yake, pia toka tumekuja hapa tumepata madini mengi ya kiroho hivyo tutayapeleka huko kwenye maeneo yetu tukaielimishe jamii yetu iweze kumjua Mungu na kusimama katika maadili mema.
Mchungaji Goodluck Daud wa kanisa la EAGT Songambele Kitangili, ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya Class Gosple Messangers (CGM) ambao ni wajumbe wa injili wa Yesu kristo jimbo la Shinyanga, lengo la kusanyiko hilo ni jinsi gani vijana wajue kujitegemee na kumwishia Mungu, kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanakaa na jamii ambayo imechanganyika na dunia, hivyo tunawafundisha ni jinsi gani kijana ataepukana na dhambi zinazomhusu kijana.
" Vijana wengi wameporomoka katika maadili ya kijamii nawashauri wazingatie elimu ya Mungu inayotolewa kwani hakuna sayansi ama njia inayoweza kumrudisha kwa Mungu, lakini kwenye elimu ya Mungu ndipo kijana anaweza akarudishwa kwenye misingi ya imani inayoendana na jamii katika ulimwengu huu, ninawashauri wamjue Mungu ili wapate amani na watimize malengo yao hapa duniani, amesema Daud.
Baadhi ya vijana waliopata mafunzo hayo akiwemo Rehema Varelian Kuziwa amesema yeye kama kijana amejifunza somo la ikimbie zinaa, ambayo ni dhambi inatendeka ndani ya mwili, maana biblia inasema "tusiliharibu hekalu la Mungu, pia tumejifunza elimu ni ya msingi kwani inafungua fahamu na kuwa na maarifa mbalimbali, niwasihi vijana wazidi kutafuta maarifa katika kusoma vitabu mbalimbali.
Kongamano hilo lilianza june 23, /6/2025 linatarajiwa kufungwa june 27 mwaka huu, ambapo mpaka sasa ni zaidi ya vijana 500 wamekusanyika kwenye kongamano hilo kwa ajili ya kupata elimu ya kiroho,na lengo la kongamano hilo ni jinsi gani vijana wajue kujitegemee na kumwishia Mungu, kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanakaa na jamii ambayo imechanganyika na dunia, ni jinsi gani kijana ataepukana na dhambi zinazomhusu kijana na kuelimisha jamii

Katbu wa jimbo la Shinyanga Jonas Samayytu akizungumza na vijana wa CGM kwenye kongamano hilo

Mchungaji Goodluck Daud wa kanisa la EAGT Songambele Kitangili, ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya (CGM) ambao ni wajumbe wa injili wa Yesu kristo jimbo la Shinyanga

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464