
Na Suzy Butondo Meatu
Mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya Jambo iliyopo Ibadakuli mkoani Shinyanga Salum Khamis Salum amejitokeza kutia nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Meatu mkoani Simiyu.
Ikiwa ni takriban siku mbili tangu dirisha lifunguliwe kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua fomu ili kushiriki katika uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo Salum Khamis amewahi kuhudumu katika nafasi za ubunge katika jimbo hilo katika vipindi tofauti tangu mwaka 2005 alipogombea rasmi ubunge wa jimbo hilo.
Salum Khamis ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi (CCM) amekuwa akishika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama chake tangu pale mwaka 2000 alipokuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa na hadi sasaakiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa pamoja na kuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa.
Fomu hizo za ugombea zimetolewa na katibu wa chama hicho Naboth Manyonyi wilayani Meatu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464