` MANISPAA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI

MANISPAA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI

MANISPAA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imepata Hati Safi,katika kwa mwaka wa fedha 2023/2024,unaoishia Juni 30,2024.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 12, 2025 na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Manispaa ya Shinyanga CPA Peter Tarimo, wakati akiwasilisha majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani,kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Alexius Kagunze.

Amesema katika mwaka huo wa fedha,CAG aliibua hoja 31, ambapo hoja 3 tayari zimetekelezwa kikamilifu na kufungwa, huku hoja 28 zikiendelea kufanyiwa kazi na Menejimenti kwa kuwasilisha majibu na vielelezo kwa Mkaguzi Mkuu wa Nje kwa ajili ya uhakiki,na kwamba wamepata Hati Safi.
“Mwenyekiti kwa kipindi cha kuishia terehe 30 Juni 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ilifunga hesabu zake na kuziwasilisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,na kutokana na Hesabu hizo Halmashauri imepata Hati Safi,”amesema CPA Tarimo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana,ameipongeza Manispaa hiyo kwa kupata Hati Safi, huku akisisitiza katika hoja 28 ambazo zimesalia vielelezo vyake vipatikane na kuhakikiwa ili hoja hizo zipate kufungwa.
Mkaguzi wa Nje CPA Yusuph Mabwe,naye ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi, na kwamba Hati hiyo imetokana na usimamizi madhubutu wa utekelezaji wa shughuli za Halmashauri na Rasilimali za Umma ipasavyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwenye Baraza hilo la hoja za CAG,amepongeza kwa Hati hiyo Safi,huku akitoa siku 7 kuanzia kesho, kwamba vielelezo vipatikane kwenye hoja 28 ambazo utekelezaji wake unaendelea ilizipate kufungwa.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko,amesema kwamba maelekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi,kwa utafutaji wa vielelezo sababu hoja zote zinajibika,huku akiwataka Wakuu wa Idara kwamba kila mmoja hoja yake ambayo inamhusu aitafutie vielelezo.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza.
Mkaguzi wa Nje CPA Yusuph Mabwe akizungumza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Manispaa ya Shinyanga CPA Peter Tarimo akiwasilisha taarifa ya CAG kwenye Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464