SALOME MAKAMBA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE VITIMAALUM CCM SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mbunge Salome Makamba,amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga,kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.
Amechukua fomu hiyo leo Juni 29,2025 katika Ofisi za Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Shinyanga,na kukabidhiwa na Katibu wa Jumuiya hiyo Habiba Musimu,na kisha kusubili taratibu zingine za Kichama.
Mbunge Salome Makamba (kulia)akikabidhiwa Fomu ya Kugombea Ubunge wa Vitimaalum CCM Mkoa wa Shinyanga na Katibu wa UWT Mkoa Habiba Musimu.
Awali Mbunge Salome Makamba akiwasili kwa usafiri wa Baiskeli kwenye Ofisi za UWT Mkoa wa Shinyanga,kwa ajili ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Vitimaalum CCM Mkoa wa Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464