` ALIYEMTIKISA KISHIMBA 2020 JIMBO LA KAHAMA MJINI ARUDI TENA KUTIA NIA 2025

ALIYEMTIKISA KISHIMBA 2020 JIMBO LA KAHAMA MJINI ARUDI TENA KUTIA NIA 2025


Mbobevu wa duru ya kisiasa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Meneja wa Rasilimali Watu wa benki ya CRDB Kanda ya ziwa Ndugu Benjamin Lukubha Ngayiwa amejitokeza tena kuwania nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2020 Ndugu Ngayiwa alimtikisa vilivyo Mbunge aliyemaliza muda wake ambapo alikuwa mtu wa pili nyuma ya Mh. Jumanne Kishimba kwa tofauti ya kura chache.


Taarifa zilizotufikia zinasema Ndugu. Benjamin Lukubha Ngayiwa ambaye ni msomi na mbobevu wa mambo ya siasa na utawala Juni 28,2025 alifika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilayani Kahama kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya Wanachama wenzake wa CCM ili wamchague kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika kinyang'anyiro cha ubunge Jimbo la Kahama Mjini.

Ndugu. Ngayiwa ambaye anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Mhe. Kishimba amesema kwamba;  "Muda muafaka ukifika ataweka wazi sababu na nia iliyomsukuma kurudi tena Jimboni kuomba ridhaa ya wananchi"
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464