RICHARD MASELE ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO JIPYA LA ITWANGI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Richard Rafael Masele,amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo Jipya la Itwangi wilaya ya Shinyanga.
Amechukua fomu hiyo leo Juni 28,2025 katika Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini.
"Leo nimechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo Jipya la Itwangi,na ninasubili taratibu zingine za kichama na jina langu likirudi kati ya majina matatu nitazungumza zaidi,"amesema Masele.
Aidha, nyazifa alizoshika Masele ndani ya Chama ni Katibu wa Vijana Tawi la Didia,Katibu Mwenezi Tawi la Didia, Katibu wa CCM Kata ya Didia,Mjumbe wa Halmshauri wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Mkoa na Katibu Siasa na Uenezi CCM Mkoa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464