` HUDUMA ZA KIBINGWA MATIBABU YA MACHO ZIMEANZA RASMI KUTOLEWA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

HUDUMA ZA KIBINGWA MATIBABU YA MACHO ZIMEANZA RASMI KUTOLEWA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Huduma za kibingwa matibabu ya macho zimeanza rasmi kutolewa Hospitali ya Rufaa Shinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

HUDUMA za kibingwa za matibabu ya macho,zimeanza kutolewa rasmi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Huduma hizo zimeanza kutolewa leo Juni 2,2025, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi.

Daktari Bingwa wa Macho Dk. Paul Kabuche, amesema kuanzishwa kwa huduma hizo ni fursa muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani,huku akiwahimiza wajitokeze kwa wingi kufika hospitalini hapo kwa uchunguzi na matibabu ya macho.
“Huduma tunazotoa ni uchunguzi wa macho,matibabu ya mzio wa macho (macho kuwasha au Allergy), mtoto wa jicho (Cataract), presha ya macho (Glaucoma),na saratani ya macho kwa watoto,” amesema Dk. Kabuche.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma hiyo, akiwemo Gerald Rubeni, wameeleza kufurahishwa kwa kuanzishwa kwa huduma hizo, wakisema zimewasaidia kuepuka safari ndefu na gharama kubwa za kwenda Hospitali ya Bugando au Muhimbili kupata huduma hizo za kibingwa.
Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk.John Luzila, amesema kwamba serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,imenunua vifaa tiba ya kisasa kwa ajili ya kuanzishwa huduma za kibingwa za macho katika hospitali hiyo, vyenye thamani ya sh.milioni 79.

TAZAMA PICHA👇👇
Daktari Bingwa wa macho Paulo Kabuche akifanya uchunguzi na kutoa matibabu ya macho kwa mgonjwa.
Ness wa Macho Jackline Elias akifanya uchunguzi wa tatizo la Macho.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464