LIGI YA MAJI CUP 2025 YATAMATIKA KASHWASA,SHUWASA WAMEFUZU KWENDA KUCHEZA FAINALI TANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Ligi ya Maji CUP 2025 Kanda ya Ziwa imetamatika, huku Timu kutoka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira KASHWASA pamoja na SHUWASA, zikifuzu kwenda kushiriki mashindano ya Ligi hiyo Kitaifa Jijini Tanga.

Ligi hiyo imeshindanisha Timu kutoka Mamlaka za Maji, ambayo imeandaliwa na Taasisi ya watoa huduma za Maji Nchini ATAWAS, kwa kushindanisha Timu za Mamlaka hiyo kutoka Kanda 8 ambapo Jana na leo mashindano hayo yalikuwa Kanda ya Ziwa, na kuchezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage.
Mtendaji Mkuu wa ATAWAS Costantino Chiwaligo, ambaye ndiye mratibu wa mashindano hayo, amezitaja Timu kutoka KASHWASA na SHUWASA kwamba ndiyo zimefuzu kwenda kucheza fainali ya Ligi hiyo Jijini Tanga ambapo watakutana na Timu zingine ambazo nazo zimefuzu kwenye Kanda zao.
“KASHWA na SHUWASA ndiyo wamefuzu kwenye kushiriki Fainali ya Ligi hii ya Maji CUP 2025 Jijini Tanga, na watakutana na Timu zingine ambazo zimefuzu kwenye Kanda zao na kutakuwa na mitoano hatu za makundi,Robo Fainali,Nusu Fainali hadi kuingia Fainali na kisha mshindo mmoja kupatikana,”amesema Chiwaligo.
Aidha, amesema mashindao ya fainali hiyo huko Jijini Tanga, itaanza kuchezwa kuanzia Julai 12 hadi 22 mwaka huu, na kwamba lengo la Mashindano haya ni kuangazia mafanikio ya Sekta ya Maji chini ya Utawala wa Awamu ya Sita.
Naye Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Mhandisi Yusuph Katopola, amesema mashindano hayo yamekuwa chachu kubwa kwa kupeleka ujumbe kwa jamii, juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji,miundombinu,na kuzuia uvujaji wa maji.
Amewataka wananchi wa Shinyanga kwamba wawe mstari wa mbele kutunza vyanzo vya maji kikiwamo chanzo cha Maji Bwawa na Nhing’hwa kwa kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ikiwamo kilimo na uvuvi, huku akiwasihi pia kutunza miundombinu ya maji, pamoja na kutoa taarifa pale wanapona kuna mivujo ya maji mahali, ili wafike mapema na kuidhibiti.
Katika hatua nyingine ameelezea mafaniko ya Sekta ya Maji ndani ya miaka 4 ya Serikali ya awamu ya Sita, kwamba Rais Samia kwa kipindi hicho ameto zaidi ya sh.bilioni 9 kwenye Mamlaka hiyo na kutekelezwa miradi ya maji 11,na kusababisha huduma ya maji kwa wananchi wa Shinyanga kufika asilimia 92.
Amesema mbali na fedha hizo pia zimetolewa fedha zingine UERO Milion 76, kwa ajili ya kutekeleza mradi wa majisafi na usafi wa mazingira, mradi ambao utamaliza shida ya maji kwa wakazi wa Shinyanga pamoja na miji ya Tinde, Didia na Iselamagazi wilayani Shinyanga.
Kwa upande wa makocha Timu hizo mbili KASHWASA na SHUWASA, wamesema wamejiandaa vyema kwenye kushiriki mashindano ya ligi hiyo ya maji, na kuahidi kurudi na kombe.
Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza.
Kocha wa Timu ya KASHWASA Michael Mgeta akizungumza.
Kocha wa Timu ya SHUWASA John Ndahani akizungumza.

Wachezaji wa Timu ya KASWASA katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa Timu ya SHUWASA katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Yusuph Katopola.