` NHAMANILO :WAPUUZENI VIONGOZI WANAOWACHUMIA VIONGOZI WENZAO NA MJIEPUSHE NA MAKUNDI

NHAMANILO :WAPUUZENI VIONGOZI WANAOWACHUMIA VIONGOZI WENZAO NA MJIEPUSHE NA MAKUNDI

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza na viongozi wa UWT na kamati ya Siasa kata ya Ngokolo

Suzy Butondo,Shinyanga

Mwenyekiti wa Umoja wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo amewataka viongozi wote wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini kujiepusha na makundi ambayo yanaweza kusababisha mpasuko ndani ya jumuiya na chama 
ikiwa ni pamoja na kuwapuuza baadhi ya viongozi wanaowachumia viongozi  wenzao.

Hayo ameyasema leo akiwa katika kata ya Ngokolo na Ndembezi wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya kutembelea kata kwa kata katika wilaya ya Shinyanga, inayolenga kuimarisha uhai wa jumuiya na chama.

Nhamanilo amesema kuna baadhi ya viongozi wanakuwa na makundi ambayo hayajengi chama badala yake yanabomoa hivyo viongozi hao waache kuendeleza makundi hayo badala yake wajenge umoja, mshikamano na upendo katika jumuiya na chama.

"Niwaombe viongozi wenzangu mdumishe amani na upendo kugombana sio afya, kionggozi mzuri ni yule anayehamasisha upendo ndani ya chama, acheni kulumbana , piia msikubali mtu awavuruge, kwani hakuna ubabe kwenye uongozi kinachotakiwa ni kuheshimiana tu"amesema Nhamanilo.

"Pia kwa muda huu niwaombe muwape ushirikiano viongozi wenu walioko madarakani,mpeni ushirikiano diwani wenu, mbunge wenu,kwani wamefanya maendeleo makubwa kwa kushirikiana na Rais Samia Suluhu, msiwazoofishe na kufuata makundi ya mifukoni achaneni nao kabisa, waacheni wafanye kazi muda ukifika mtachagua viongozi mnaowataka"ameongeza Nhamanilo.

"Sisi jumuiya tujisimamie wenyewe fanyeni kazi kwa maelekezo ya UWT waelezeni watu yaliyofanywa na chama cha mapinduzi CCM, acheni kupeleka uongo kwa wagombea semeni mema yaliyofanywa na viongozi, kwani baadhi ya wagombea wanakuja kwa ubaguzi na kutengeneza makundi ambayo yanaweza kukiuwa chama,jiepusheni na masuala ya rushwa ambayo inaweza kuwasababishia madhara makubwa"amesema

Kwa upande wake katibu wa UWT (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi amesisitiza zaidi kuhusu uhai wa jumuiya hiyo na,kuwataka kusimamia ulipaji wa ada, kusajili wanachama wapya na kusimamia kanuni na utaratibu wa jumuiya hiyo na chama.

Pia aliwahamasisha wanawake wenye sifa wajitokeze katika kuchukua fomu za kugombea nafasi za udiwani na ubunge.

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Zamda Shaban amesema kumekuwa na tabia ya kuchafuana viongozi kwa viongozi, ambapo amewaomba wasiendelee kumkaribisha shetani wa kuchafuana kwenye maeneo hayo, "tunatakiwa tubebane kwa mapungufu yetu tuwe wamoja pia, tuwatii na waume zetu tukiwatii hatuwezi kuwafanyia madhambi, sisi wamama ndiyo mwalimu wa kwanza nyumbani, tuheshimu kila mtu"
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza na viongozi wa UWT ns kamati ya Siasa kata ya Ngokolo
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza na viongozi wa UWT na kamati ya siasa kata ya Ngokolo
Katibu wa UWT (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza na viongozi wa UWT na kamati ya Siasa kata ya Ngokolo
Katibu wa UWT (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza na viongozi wa UWT na kamati ya Siasa kata ya Ngokolo
Mwenyekiti wa UWT kata ya Ngokolo Hulda Masaba akizungumza
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kata ya Ngokolo George Mwandu akizungumza
Diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akizungumza
Mwenyekiti wa wazazi kata ya Ngokolo Genda Mabula akizungumza kwenye kikao cha UWT kata
Viongozi mbalimbali wa UWT na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo
Viongozi mbalimbali wa UWT na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo
Viongozi mbalimbali wa UWT na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo
Viongozi mbalimbali wa UWT na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo

Viongozi mbalimbali wa UWT na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo
Katibu wa UWT (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza na viongozi wa UWT kata ya Ndembezi
Mwenyekiti wa UWT kata ya Ndembezi Lyina Kazimily akizungumza kwenye kikao cha UWT kata ya Ndembezi
Katibu wa UWT kata ya Ndembezi akizungumza kwenye kikao cha UWT kata

Wajumbe wa UWT kata ya Ndembezi wakiburudika baada ya kumpokea mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Juliana Buzuluga akisalimia viongozi wa UWT kata ya Ndembezi
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Salome Abuolo akisalimia viongozi wa UWT kata ya Ndembezi
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mariam Kajala akizungumza kwenye kikao cha UWT Ndembezi
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa UWT kata ya Ndembezi wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Wajumbe wa UWT kata ya Ndembezi wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Katibu wa UWT (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akiwashukuru viongozi wa UWT kata ya Ndembezi kwa kuhudhulia kwenye kikao hicho
Baadaya kazi zawadi




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464