` FEDHA ZA WAKULIMA 152 KIASI CHA MILION 151 ZAFUNJWA NA VIONGOZI WA AMCOS -USHETU

FEDHA ZA WAKULIMA 152 KIASI CHA MILION 151 ZAFUNJWA NA VIONGOZI WA AMCOS -USHETU

 


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari

FEDHA ZA WAKULIMA 152 KIASI CHA MILION 151 ZAFUNJWA NA VIONGOZI WA AMCOS -USHETU

Na Estomine Henry.

Viongozi wa chama cha msingi Ibambala Halmashauri ya ushetu, wilayani kahama mkoani Shinyanga  wamebainika kugawana fedha za wakulima wapatao 152 sawa na kiasi cha shilingi milioni 151.53 zilizotolewa na kampuni ya Alliance One kama fidia kwa wakulima wa zao la tumbaku waliopata hasara kutokana na mafuriko yaliyotoekea katika msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 na kusababisha hasara.

Hayo yameelezwa leo Mei 27, 2025 na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy wakati akiwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya kipindi cha januari hadi machi kwa mwaka 2024/2025 kupitia vyombo vya habari.

“TAKUKURU imebaini kuwa kiasi kikubwa cha fedha, shilingi milioni 151.53 kiligawiwa kwa watu wasio stahili, wakiwemo ndugu wa viongozi hao” amesema Kessy

Kessy amesema, TAKUKURU ilibaini kuwa shilingi milioni 11.62 zilichukuliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa matumizi yao binafsi, akiwemo Katibu Meneja Bw. Charles Alex Shiyengo na Mwenyekiti Bi. Faida Paulo Deva

"Miongoni mwa waliopokea fedha hizo ni Bi. Lucy Masanja Gidabita, mke wa Katibu Meneja, ambaye alipokea shilingi milioni 34.58, pamoja na Bw. Charles Charles Masanja aliyelipwa shilingi milioni 5.58.

Kessy amesema hatua za awali za kurejesha fedha hizo zimeanza kuchukuliwa huku wahusika wakikabiliwa na hatua za kisheria",ameongeza

Kwa upande mwingine,Takukuru Shinyanga pia imepokea jumla ya taarifa 57 za tuhuma za rushwa, ambapo 52 zilifanyiwa uchunguzi na 13 kati yake zimefikishwa mahakamani.

Vile vile, Taasisi hiyo imeweza kutoa wa elimu kwa umma kwa kuendesha imeendesha mikutano ya hadhara 61, semina 30, na vipindi vya redio na runinga 13 kupitia programu yao ya Takukuru Rafiki, lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

 


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464