` UJUMBE WA "SCAN CODE TO APPLY" YA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO WAFIKA SHULE YA SEKONDARI ENDASAKI MKOANI MANYARA

UJUMBE WA "SCAN CODE TO APPLY" YA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO WAFIKA SHULE YA SEKONDARI ENDASAKI MKOANI MANYARA


Ujumbe wa "Scan code to Apply" ya Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wafika Shule ya Sekondari Endasaki (High School) Mkoani Manyara.
Ujumbe huo umefikishwa na Afisa Habari wa Chuo hicho Josephine Charles wakati alipotembelea shule hiyo kutoa Elimu ya kozi wanazofundisha ili mwanafunzi aweze kusoma kwa malengo ya kuja kuwa nani, kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi kwa kuwa serikali ya Tanzania inatoa mikopo kwa kozi za Radiology, Physiotherapy na Medical Laboratory pamoja na kuwaomba kutuma maombi ya kujiunga na Chuo hicho kwa kuscan code au kupiga simu namba 0742155623.

Aidha chuo hicho kinafundisha kozi 8, Sita zikiwa niza Afya na mbili zikiwa niza ufundi ambazo ni pamoja na Clinical Medicine, Nursing and midwifery, Pharmaceutical sciences, Medical Laboratory, Physiotherapy na Radiology na Kozi za Ufundi ni Laboratory Assistant na Computer.

Hata hivyo wanafunzi wote wenye vigezo vya kusoma fani za Afya na Ufundi wametakiwa kutuma maombi mapema kwa kuwa ni huu ndiyo muda sahihi wa kutuma maombi hayo.
 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464