KATAMBI AENDELEA KUTOA FEDHA KUENDELEZA MICHEZO YA JADI

KATAMBI AENDELEA KUTOA FEDHA KUENDELEZA MICHEZO YA JADI

Na Marco Mduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,ametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya kuendeleza michezo ya Jadi.

Fedha hizo zimekabidhi wa leo Mei 8,2025 na Mwalimu Yusuph Mbundi,kwa viongozi wa Michezo hiyo ya Jadi Manispaa ya Shinyanga, kwa niaba ya Mbunge Katambi.
Mwalimu Yusuph Mbundi (kushoto)akikabidhi fedha kwa niaba ya Mbunge Katambi.

Amesema michezo hiyo ya Jadi Katambi ndiyo Mdhamini wake,na itagharimu zaidi ya shilingi milioni 6, na kwamba awali walishatoa shilingi milioni 3, na sasa amekabidhi tena shilingi milioni 1.5, fedha ambazo zitaendeleza mashindano ya michezo hiyo ambayo bado yanaendelea katika Kata za Manispaa ya Shinyanga.

“Kwa niaba ya Mbunge Katambi nakabidhi shilingi milioni 1.5 kwa viongozi wa michezo ya Jadi Manispaa ya Shinyanga,fedha ambazo zitaendeleza michezo hii na kuenzi utamaduni wa Mwafrika,”amesema Mbundi.
“Nampongeza Mbunge Katambi kwa kufufua michezo hii ya Jadi, ambayo ipo kwenye utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM, nawaomba tu wananchi waendelee kumuunga mkono Mbunge wao, pamoja na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ya kuwaletea maendeleo,”ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Michezo ya Jadi wa Manispaa ya Shinyanhga Janeth Seseja,amemshukuru Mbunge Katambi kwa kuiendeleza michezo ya jadi na kufufua utamaduni ambao ulikuwa umepotea.
“Mungu ambariki sana Mbunge Katambi kwa kufufua utamaduni wetu, na maeneo ambayo tayari tumeshafika wakati wa michezo hii ya Jadi,wananchi wamefurahi sana kuona utamaduni wao ukienziwa,tunamshukuru mno Mbunge wetu ana guswa na maisha ya wananchi wake,”amesema Janeth.

Aidha,Mashindano hayo yanafahamika kwa jina la "Katambi na Jadi wilaya ya Shinyanga Mjini"
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464