BUTONDO AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI NGOFILA NA LAGANA,AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Marco Maduhu,KISHAPU
MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ameendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya wamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini,ambapo amekabidhi vifaa vya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kwa shule za Sekondari Ngofila na Lagana.
Amekabidhi vifaa hivyo jana katika shule hizo kwa nyakati tofauti, huku akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, amesema lengo lake ni kuunga mkono Juhudi za Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, za kuboresha sekta ya elimu,ili wanafunzi wasome kwa vitendo na kupata ufaulu mzuri.
“Vifaa vya TEHAMA ambavyo nimetoa ni Kompyuta, Seti nzima, Mashine ya kuchapisha (Printer),CPU na Projector, vitakavyo saidia uinuaji wa taaluma kwa wanafunzi,”amesema Butondo.
“Vifaa hivi vitawasaidia pia Walimu katika maandalizi ya masomo pamoja na kuchapa Mitihani,hakuna tena kwenda kwenye Stationary za watu binafsi, pia itapunguza na gharama za uaandaaji wa mitihani,”ameongeza.
Aidha,ametoa maelekezo kwamba,vifaa hivyo vitunzwe pamoja na kuzingatiwa usafi, sambamba na kuanzishwa masomo ya Computer hasa katika shule ya Lagana ambayo haina somo hilo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Ngofila Matrida Mwaliaje, amesema vifaa hivyo vya TEHAMA ni chachu kubwa ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, sababu watavitumia kuchapisha mitihani mara kwa mara kwa kuwapatia majaribio wanafunzi na kujua uwezo wao na kuongeza bidi zaidi za ufundishaji.
Amesema vifaa hivyo pia vimewaepusha na gharama kubwa ya kwenda kuchapisha mitihani katika shule kubwa ikiwamo ya Kishapu na Ukenyenge umbali wa kilomita 60, lakini sasa hivi watakuwa wakichapisha mitihani hapo hapo shuleni.
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Lagana Adam Malongo, ameshukuru kwa vifaa hivyo vya TEHAMA,kwamba ni msaada mkubwa kwa ustawi wa elimu.
Nao baadhi ya wanafunzi akiwamo Hadija Pambe,amesema vifaa hivyo ni msaada mkubwa katika masomo yao, sababu watakuwa wakisoma kwa vitendo na kupewa majaribio ya mitihani mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu, amempongeza Mbunge Butondo kwa kuendelea kuunga mkono suala ya elimu,kwamba amekuwa akiitekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Vitendo.
Aidha, Mbunge Butondo tayari ameshatoa vifaa vya TEHAMA katika Shule Tatu za Sekondari Jimboni humo, ikiwamo Kishapu Sekondari, Ngofila na Lagana.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye hafla ya Mbunge Butondo kukabidhi Vifaa vya TEHAMA katika shule za Sekondari Ngofila na Lagana.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA.
Mkuu wa shule ya Sekondari Ngofila Matrida Mwaliaje akizungumza.
Mwanafunzi Hadija Pambe akishukuru.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kushoto)akimkabidhi Vifaa vya TEHAMA Mkuu wa shule ta Sekondari Ngofila Matrida Mwaliaje.


Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kushoto)akimkabidhi Vifaa vya TEHAMA Mkuu wa shule ta Sekondari Ngofila Matrida Mwaliaje.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa na Mwanafunzi Happy wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondari Ngofila.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kushoto)akimkabidhi vifaa vya TEHAMA Mkuu wa shule ya Sekondari Lagana Adam Malongo.


Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464