BUTONDO ATAJA MAAJABU YA MAENDELEO JIMBO LA KISHAPU NDANI YA MIAKA MINNE YA RAIS DK. SAMIA MADARAKANI
Na Marco Maduhu,KISHAPU
MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ameelezea mapinduzi makubwa ya kimaendeleo ambayo yamefanyika katika jimbo hilo ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwamba haijawahi kutokea.
Amebainisha hayo jana kwenye Mkutano wa hadhara wa Katibu wa Nec Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makala wakati akizungumza na wananchi wa Maganzo wilayani Kishapu.
Amesema ndani ya miaka minne ya Rais Dk.Samia madarakani,kwamba wilaya hiyo ya Kishapu imepiga hatua kubwa kimaendeleo ikiwamo utekelezwaji wa miradi mingi ya maendeleo na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili wananchi.
“Chama chetu kimetutendea haki sana Kishapu,mfano ndani ya hii miaka minne ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,tumejenga shule 3 mpya ya Sekondari, ikiwamo na kuweka madawati na hakuna mwananchi ambaye amechangishwa pesa yoyote,”amesema Butodo.
“tumejenga pia shule mpya ya msingi, pamoja na kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu,”ameongeza.
Amesema kwa upande wa sekta ya maji kwamba kabla ya kuwa Mbunge kulikwa na Kata 3 tu zenye maji huduma ya majisafi na salama, lakini sasa hivi Kata ambazo zinahuduma hiyo zimefika 21 na kusalia Kata 8 na kwamba bado kuna miradi ya maji inaendelea kutekelezwa.
Butondo amezungumzia pia kwa upande wa miundombinu ya barabara kwamba mwaka 2021 kulikwa na Kilomita 675 za mtandao wa barabara,lakini sasa hivi zimefika kilomita zaidi ya 1,000.
Amezungumzia pia huduma ya umeme kwamba kulikuwa na vijiji 48 tu,lakini sasa vimefikiwa vijiji 117,huku akibainisha kuwa kwa upande wa mawasiliano kwamba Kata ambazo zilikuwa na huduma hiyo ni 4 lakini sasa Kata zote zina Mawasiliano.
Aidha,amesema kwa upande wa huduma za afya kwamba zimejengwa Zahanati,Vituo vya Afya pamoja na kuendelea kuboreshwa Hospitali ya wilaya ya Kishapu na upatikanaji wa vifaa tiba zikiwamo gari za wagonjwa Ambullance.
“Mambo ni mengi sana ya kimaendeleo,ambayo ameyafanya Rais Samia katika Jimbo hili la Kishapu na sisi Kama Wabunge tukimsaidia,tunacho muahidi sisi katika Jimbo la Kishapu ni ushindi wa Kishindo kwenye sanduka la kura,”amesema Butondo.
Kwa upande wake Katibu wa Nec Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makalla, amekiri wazi kwamba Kishapu ambayo alikuwa akiifahamu miaka ya nyuma kwamba siyo ya sasa sababu imepiga hatua kubwa kimaendeleo.
“Nakumbuka nilipokuwa Naibu Waziri wa Maji nilikuja Kishapu, enzi hizo Mkuu wa wilaya alikuwa Willison Nkambaku,kulikuwa na shida kweli ya maji,lakini sasa hivi zimebaki 8 tu ambazo hazina maji haya ni mapinduzi makubwa ya kimaendeleo,”amesema Makalla.
Aidha, amewataka wananchi wa Kishapu kwamba siku ya uchaguzi Mkuu wasifanye makosa bali wakawachague viongozi wote wanaotokana na CCM ambao ndiyo watakao waletea maendeleo kama ilivyo sasa.
TAZAMA PICHA👇👇
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makalla akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia)akiwa na Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464