Wanafunzi wameshauriwa kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kusoma fani za Afya kwa kuwa fani hizo zinahitaji ufaulu wa masomo ya Sayansi.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Habari wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga Josephine Charles alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Measkron Mkoani Manyara katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea shule mbalimbali za Sekondari mkoani humo.
Amewaambia wanafunzi kuwa ukitaka kuwa Daktari, Muuguzi, Mtaalamu wa Maabara, Mtaalamu wa Dawa, Mtaalamu wa Mionzi au Mtaalamu wa Mazoezi Tiba ni lazima usome masomo ya Sayansi na ufaulu.
"Napokea simu mbalimbali za wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo chetu na wakitaka kusoma fani za Afya lakini ukianza kumsajili ukifika kipengele cha matokeo ya masomo yake katika masomo ya Sayansi aliyosoma ni Biology tu na bado amefeli, hivyo nimewaomba pia waalimu wa shule hizo kutumia walau dakika moja darasani kabla hawajaanza kufundisha kuwapa elimu wanafunzi kuwa wakitaka kuwa wataalamu wa Afya basi wanatakiwa kusoma masomo ya Sayansi na kufaulu" amesema Josephine.
Mbali na kutoa ushauri pia amewakaribisha wanafunzi hao Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kusoma Fani za Afya zikiwemo Clinical Medicine, Nursing & Midwifery, Physiotherapy, Medical Laboratory, Pharmaceutical Sciences na Radiology. Pia kusoma Fani za Ufundi zikiwemo Laboratory assistant na Computer.
Amewaeleza pia mikopo inayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wanafunzi wa vyuo vya Afya vya kati wanaosoma kozi za Radiology, Physiotherapy na Medical Laboratory; Hivyo amewataka wanafunzi wote kusoma kwa malengo na kuchangamkia fursa ya mikopo ili kupunguza gharama za maisha pindi wanapokuwa kwenye masomo chuoni.
Aidha Chuo hicho kinapatikana Mkoa wa Shinyanga, Mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Simiyu, hivyo kwa wote wenye ufaulu wa masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya kidato cha nne wameombwa kujiunga na Chuo hicho kwa kupiga simu 0742155623, kutembelea tovuti ya chuo www.kchs.ac.tz au kwa kuscan code kupitia QR Code au kufika Chuoni.