` UJUMBE WA"SCAN CODE TO APPLY CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO WAFIKA SHULE YA MARY NAGU MKOANI MANYARA

UJUMBE WA"SCAN CODE TO APPLY CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO WAFIKA SHULE YA MARY NAGU MKOANI MANYARA

Ujumbe wa "Scan Code to Apply" ya Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wafika Shule ya Mary Nagu Sekondari iliyopo Mkoani Manyara.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Habari wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Shinyanga Josephine Charles katika mwendelezo wa ziara yake ya kufikisha ujumbe wa "Scan Code to Apply" ya chuo hicho katika shule za Sekondari zilizopo Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.

Amesema amekutana na changamoto nyingi za wanafunzi kutaka kusoma fani za Afya huku wakiwa hawana vigezo vya kusoma kutokana na kukimbia masomo ya sayansi wakiwa shule za Sekondari pamoja na kutokujua kama masomo ya sayansi ndiyo yatamwezesha kusoma fani za afya.

Amesema wao kama Chuo cha Afya Kolandoto wameamua kutembelea shule za Sekondari kutoa Elimu, kuhabarisha pamoja na kuwatangazia fursa mbalimbali zinazotokana na ufaulu wa masomo ya Sayansi pamoja na kusoma fani za Afya.

Amewaomba wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mary Nagu kuwafikishia ujumbe wenzao waliohitimu miaka ya nyuma kuwa wajiunge na masomo kwa 2025/2026 kwa Fani za Afya naza Ufundi.

Ameeleza Fani za Afya zinazofundishwa Chuoni hapo zenye mkopo wa Serikali ni pamoja na 'Medical Laboratory, Radiology na Physiotherapy' na zingine ni 'Nursing & midwifery, Pharmaceutical Sciences na Clinical Medicine. Na fani za Ufundi ni 'Laboratory Assistant na Computer'.

Hata hivyo amesisitiza kuwa wanafunzi wote wenye vigezo vya kusoma fani hizo wanatakiwa kutuma maombi kwa njia ya ku Scan code au kupiga simu namba 0742155623 au kufika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga.

Katika hatua nyingine amewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mary Nagu iliyopo Mkoani Manyara kusoma masomo ya Sayansi ili kuweza kuwa wataalamu wa Afya.

Aidha Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Shinyanga kina matawi yake Mkoani Mwanza na Simiyu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464