RC MACHA:SERIKALI ITASHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI MOJA BAADA YA NYINGINE

RC MACHA:SERIKALI ITASHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI MOJA BAADA YA NYINGINE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SERIKALI Mkoani Shinyanga,wimeahidi kuzitatua changamoto zote ambazo zinawakabili wafanyakazi wa Mkoa huo moja baada ya nyingine.
Hayo yamebainishwa leo Mei 1,2025, na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,wakati akitoa hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi mkoani humo, ambayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya CCM Kambarage.

Amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa zitafanyiwa kazi moja baada ya nyingine,ili kwenye maadhimisho ya mwakani zisiwepo tena na kubaki kuwa historia.
“Changamoto zote ambazo zinawakabili wafanyakazi zilizowasilishwa hapa ziwezi kuzitolewa majibu, bali na muagiza Katibu Tawala wa Mkoa,aunde Timu ya watu kati ya Watano hadi Sita,vikiwamo na Vyama vya Wafanyakazi, ili changamoto moja baada ya nyingine ishughulikiwe,na hata kuwafikia Waajiri ambao wanalalamikiwa Mmoja baada ya mwingine,”amesema Macha.

Amewataka Wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa bidii na weledi, na kwamba Serikali chini ya Rais Dk.Samia ipo kazini, na tayari ilishatoa Ajira mpya,Watumishi kupandishwa madaraja, na itaendelea pia kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi.
Aidha,amewataka wananchi pamoja na wafanya kazi, kwamba wajitokeze kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, zoezi ambalo tayari limesha anza mkoani humo na litadumu kwa siku 7.

Amewataka pia Wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu, na kupuuza matamko ya Chama Kimoja cha Siasa, ambacho kinatoa masharti ya uchaguzi huo, na kwamba uchaguzi upo pale pale, na hakuna mtu wa kuuzuia sababu upo kwa mujibu wa Katiba.
Katibu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Shinyanga Ramadhani Pangara, awali akisoma Rasala ya Wafanyakazi, ametaja Changamoto ambazo zinawakabili Wafanyakazi, kuwa tatizo la Kikokotoo limekuwa likiwanyima usingizi,na kuiomba serikali irudishe kikokotoo cha zamani cha asilimia 50.

"Tatizo la kikokotoo linatunyima usingizi, tunaomba serikali ilirudishe cha zamani cha asilimia 50,na siyo cha sasa kina tuumiza," amesema Pangara.
Ametaja changamoto nyingine ni Wastaafu kutolipwa Mafao yao kwa wakati, na kuomba wanapomaliza rikizo ya kwanza ni vyema wakapewa Mafao yao.

Nyingine ni Waajiri wa Sekta binafsi kutozingatia sheria na taratibu za ajira, na hata kutowapatia wafanyakazi wao mikataba ya kazi.
Ametaja nyingine, ni baadhi ya Waajiri kutoruhusu wafanyakazi wao kujiunga na vyama vya wafanyakazi, na wanaotaka hupatiwa vitisho na hata wengine kufukuzwa kazi.

Nyingine ni Waajiri kutopeleka michango ya Wafanyakazi wao kwa wakati kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii NSSF,pamoja na kutowapatia hati za malipo.
Waliulalamikia pia mfuko wa Bima ya Afya kupunguza baadhi ya vifufurushi, na kwamba ni kuwanyanyasa Watumishi.

Pia,walilalamikia tatizo la baadhi ya Waajiri,kutowapatia Motisha Wafanya kazi wao, na hata kuwanyima zawadi katika Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi.
Aidha,ameiomba serikali iendelee kujali maslahi ya wafanyakazi, pamoja na kutatua changamoto ambazo zinawakabili, sababu wao ndiyo Mhimili wa taifa.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi mwaka huu inasema”Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi: sote tushiriki.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Yohana Magembe akizungumza.
Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Ramadhani Pangara.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akitoa zawadi kwa Watumishi Hodari,pamoja na washindi wa Michezo ya Mpira wa Miguu na Pete.










Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464