HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA YAADHIMISHA MEI MOSI KWA KUPANDA MITI NA KUFANYA MAZOEZI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,wameadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),kwa kupanda miti 500 katika maeneo ya hospitali hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira na kuhimiza utunzaji wa afya kwa njia ya mazoezi.
Dk.Luzila John.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Aprili 30,2025, ambapo pamoja na upandaji miti, watumishi hao walishiriki mbio za kilomita 7.8 kama njia ya kuimarisha afya zao.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Luzila John, amesema kuwa wameamua kupanda miti hiyo ili kuboresha mazingira ya hospitali, pamoja na kukimbia mbio hizo ili kuimarisha afya za Watumishi, na kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi.
"Kesho ndiyo Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, ambayo Kitaifa yatafanyika Singida, lakini na sisi kama Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Rufaa hapa Shinyanga,tumeamua kupanda Miti pamoja na kukimbia Mbio kilomita 7.8 ili kuimarisha Afya zetu,"amesema Dk.Luzila.
Amesema,wameweka pia Mabanda katika Uwanja wa CCM Kambarage,kwa ajili ya wananchi kupima afya zao,huku akitoa wito kwa wananchi wapende kupima afya zao, pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara,ili wajikinge na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
“tunatarajia pia kuanzisha Shinyanga RS Fitines Club, ili Watumishi wawe wanafanya mazoezi, na hata kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao, ili wajikinge na magonjwa yasiyo ya kumbukiza,"ameongeza.
Afisa Afya Mazingira katika Hospitali hiyo Emiliana Charles, amesema katika zoezi hilo wamepanda miti 500, ambayo itasaidia pia wagonjwa kupata kivuli,matunda na kuzuia pia Mmomonyoko wa udongo.
TAZAMA PICHA👇👇
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk.Luzila John akizungumza na Watumishi.
Awali Mbio wa Kilomita 7.8 zikiendelea.
Mazoezi ya viungo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk.Luzila John akipanda Mti.
Upandaji Miti ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464