Header Ads Widget

BENARD BENSON WEREMA AMESHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA MWENYEKITI UVCCM MKOA WA SHINYANGA


Bernad Benson Werema ameibuka Mshindi nafasi ya Uenyekiti UVCCM Mkoa wa Shinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Wagombea.

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Mkoa wa Shinyanga,imefanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, ambapo Benard Benson Werema ameibuka Mshindi kwa kupata kura 252.

Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 4,2024 na kusimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka.
Benson Werema Mwenyekiti Mpya UVCCM Mkoa wa Shinyanga.

Chikoka akitangaza Matokeo hayo, amesema Wagombea walikuwa Wanne, kura zilizopigwa ni 367, kura zilizoharibika ni 6,huku kura halali ni 361.

Amemtaja Benard Benson Werema kuwa ndiyo Mshindi wa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, kwa kupata kura 252,Mshindi wa pili ni Makamba Lameck amepata kura 78, akifuatiwa na Irene Masakilija kwa kupata kura 19, huku Severen Mbulu akipata kura 12.
DC wa Rorya Juma Chikoka.

Aidha,Werema akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo amewashukuru Wajumbe kwa kumpigia kura na ameahidi atafanya kazi kwa bidii na kukipigania Chama ikiwamo kupata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo, amepongeza uchaguzi huo kwa kufanyika kwa Amani na Utulivu,huku akiwasihi Vijana kwenda kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Pia,amewahamasisha Vijana wa UVCCM kwamba wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi na ujumbe kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu.

Aidha,uchaguzi huo umefanyika mara baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Clement Madinda kujihudhuru nafasi hiyo mara baada ya kupata kazi mkoani Mbeya.

Post a Comment

0 Comments