Header Ads Widget

CAMFED WATAMBULISHA MRADI WA STADI ZA MAISHA


CAMFED WATAMBULISHA MRADI WA STADI ZA MAISHA

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na Wadau kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la CAMFED wamefika katika Ofisi ya RC Shinyanga kwa lengo la kujitambulisha wao wenyewe na kuutambulisha mradi aa Stadi za Maisha katika Shule za Sekondari za Serikali zilizopo katika Mkoa Wa Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine, RC Macha amewapongeza sana kwa utekelezaji wa kazo uku akiwaahidi ushirikiano wakati wote na kwamba Serikali inathamini na kutambua mchango wao katika jamii hasa katika kuwakwamua watoto wa kike ili waweze kufikia malengo na ndoto zao katika maishayao ya sasa na ya baadae.

"Karibuni sana mkoani Shinyanga, nawapongeza kwa kazi zenu nzuri zenye lengo la kuwakwamua watoto wa kike ili watimize ndoto zao, na Serikali inatambua na kuthamini mchago wenu kwa jamii ikiwemo ya Wanashinyanga," amesema RC Macha.

CAMFED Ni shirika lisilo la kiserikali lenye Makao Makuu yake nchini Uingereza lakini linafanyakazi katika nchi (5) tano za Afrika zikiwa ni pamoja na Ghana,Tanzania, Zambia, Malawi na Zimbabwe.

Shirika limejikita katika kumkwamua mtoto wa kike aliopo katika mazingira yenye vikwazo vinavyoweza kumkwamisha kuzifikia ndoto zake za baadae.

Mradi Wa stadi za Maisha unatarajiwa kuanza kutekelezwa kwa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa Shule za Serikali ifikapo mwezi January, 2025.

Post a Comment

0 Comments