Header Ads Widget

KASHWASA YAPATA HATI SAFI MFULULIZO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI, RC MACHA APONGEZA USIMAMIZI MZURI


Mtalaam wa ubora wa maji Kituo cha uzalishaji maji Ihelele Gerald Mghina akitoa maelezo juu ya mradi wa maji baada ya Mkuu wa Mkoa kutembelea mradi huo ambao unasambaza maji zaidi ya Mikoa mitano.

   Na Stella Homolwa,Shinyanga Press Club Blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameipongeza Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira (KASHWASA) kutokana na kutekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni  pamoja na kupata hati safi ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali(CAG).

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo katika Kijiji cha Ihelele Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Mkoa amesema kazi kubwa imefanyika ya kutunza mazingira na kuhakikisha maji yanakuwa katika ubora wa kimataifa.

Amesema mradi huo tangu ulipoanzishwa mwaka 2009 Mamlaka hiyo kila ikifanyiwa ukaguzi imekuwa ikikidhi vigezo na kupatiwa hati safi jambo ambalo linapaswa kuigwa na taasisi zingine katika kusimamia miradi yao.

“Nimeona namna ambavyo maji yanaanza kusafishwa kutoka Ziwa Victoria hadi kufikia hatua ya kuwa safi na kusambazwa kwa wateja na hatua kubwa mnastahili pongezi,mambo kama haya wananchi wetu wanatakiwa wajue,Madiwani,wabunge na kamati za watumia maji vijijini ili kujua gharama”amesema Macha

Amesema wakati mwingine gharama za maji zinapokuwa juu inatokana na mchakato mzima unaotumika kutibu maji hayo, hadi kufikia hatua ya kupelekwa kwenye tenki kuu ili kusambazwa kwa wateja.

Mkuu wa Mkoa akizungumzia changamoto ya madeni katika taasisi hiyo amesema licha ya kutoa huduma lakini bado ina zidai Mamlaka za maji ambazo zinauziwa maji na Kashwasa zaidi ya Sh bilioni 14 zikiwemo jumuiya za watumia maji ngazi ya jamii.

Changamoto ambayo imekuwa ikikwamisha   Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (Kashwasa)kushindwa kulipa deni la umeme la Tanesco zaidi ya Shilingi bilioni nne na kusababisha kusuasua.

 Amesema Kuendesha mitambo ya maji ina gharama kubwa ambapo kwa mwezi umeme pekee unagharimu Sh650 milioni,ambapo ametoa wito kwa mamlaka zote zinazodaiwa kulipa madeni yake pamoja na wananchi kulipa bili zao kwa wakati.

 Mkurugenzi wa Kashwasa Mhandisi Patrick Nzamba,amesema Kituo hicho kinauwezo wa kusafisha  na kuchakata  maji lita milioni 80 kwa siku na kwamba wamefikia Mikoa ya Mwanza,Tabora,Singida,Simiyu,Geita na Shinyanga.

Amesema kwa sasa wanatoa huduma ya maji kwa watu milioni 1.9 katika Mikoa hiyo,ambapo wana  makundi matatu zikiwemo Mamlaka za maji nane,watoa huduma za maji ngazi za jamii 95 na kundi la jingine ni migodi.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza baada ya kutembelea mradi wa maji ya Ziwa Victoria Kijiji cha Ihelele

Ziara inaendelea


          Mkurugenzi wa Kashwasa Mhandisi Patrick Nzamba akifafanua jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Kituo cha maji ya Ziwa Victoria Ihelele.
                                    


Post a Comment

0 Comments