Header Ads Widget

RC MACHA AMETOA CHAKULA CHA SIKUKUU YA EID EL FITR KAMBI YA WAZEE KOLANDOTO


RC MACHA AMETOA CHAKULA CHA SIKUKUU YA EID KAMBI YA WAZEE KOLANDOTO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, ametoa Chakula kwa ajili ya Sikukuu ya Eid Kambi ya Wazee Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Chakula hicho amekitoa leo April 9,2024 katika Kambi hiyo ya Wazee Kolandoto.

Amesema Serikali itahudumia wananchi kupitia Makundi Mbalimbali bila ya kujali hali zao na kuwapatia furaha, na kwamba ili wananchi wake wawe na furaha lazima wawe na Mahitaji yao ya kila siku, na ndiyo maana Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imeamua kuwapatia Chakula wazee hao ili wafurahie Sikukuu ya Eid.
“Wazee hawa katika Kambi ya Kolandoto tumewapatia Mchele Kilo 100, Maharage Kilo 20, Mafuta ya kupikia, Juice, Chumvi, Sabuni za Unga, pamoja na kuwapatia fedha kwa ajili ya kununua Nyama,”amesema Macha.

Nao Wazee hao Emmanuel Medard,wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, kwa kuwapatia Chakula hicho kwa ajili ya Sikukuu ya Eid.
Mlezi wa Kituo hicho Sophia Kang’ombe, amesema Kituo hicho kina Wazee 18 na wamekuwa wakiwapatia huduma mbalimbali yakiwamo Malazi na Matibabu.
Chakula cha Sikukuu ya Eid ambacho kimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.

Post a Comment

0 Comments