Header Ads Widget

MWANAMKE MMOJA ABAKWA NA KUKATWA MKONO ARUSHA


Mwanamke mmoja abakwa na kukatwa mkono Arusha

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jescah Mneli mfanyabiashara mdogo wa viazi na mkazi wa Kijiji cha Orkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amekumbwa na tukio la kilatili mara baada ya vijana watatu ambao ni wafanyabiashara wenzake kumbaka na kisha kumkata mkono.


Jescah Mneli ambaye amekumbwa na tukio la kikatili kutoka kwa vijana watatu ambao ni wafanyabiashara wenzake kwa kumbaka na kisha kumkata mkono.


Tukio hilo linadaiwa kutokea Jumamosi ya Aprili 04, 2024 ambapo mwanamke huyo alipokutana na vijana ambao ni wafanyabiashara wenzake kisha kuelekea kwenye shamba la viazi ili kupanga bei na ndipo vijana hao wakamkamata kwa nguvu mama huyo kisha kumbaka na kumkata mkono.

Bi. Jescah anaiomba Serikali na wadau wengine kumsaidia kupata haki zake na kumudu gharama za matibabau wakati huu ambao anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Seriani

Daktari Robert Julius ambaye anaendelea kumpatia matibabu mama huyo amesema kwa sasa anaendelea vizuri licha ya kuwa bado ana maumivu.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO EATV

Post a Comment

0 Comments