ASKOFU SANGU;Kukosekana upendo katika familia na kushindwa kusamehana imetajwa kuwa ni chanzo cha ndoa nyingi kushindwa kudumu.
Stella Homolwa,SHINYANGA
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewataka wananchi waishi kwa kusameheana katika maisha yao na kwamba ndoa nyingi zitapona.
Amesema ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika pamoja na familia kurafaka ni kutokana na watu kuishi bila ya kusameheana.
Amebainisha hayo leo Machi 29,2024 kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Kanisa Katoliki la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo.
Askofu Sangu amesema wanapotafakari mateso ya bwana yesu kristu dhamira zetu ziendelee kutusuta tunapotenda zambi tuwe na hofu ya mungu na tuwe watu wa msamaha katika familia zetu hatua ambayo itasaidia kulinda ndoa nyingi zitadumu pia katika jumuiya zetu tuwe watu wa msamaha.
Amesema mara nyingi wakinamama ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuomba msamaha katika familia lakini walinababa wengi hatuombi msamaha,ambapo amesisitiza kuwa msamaha unasaidia kulinda ndoa na kudumu.
Amesisitiza kuwa watu wa upendo kama ilivyo kwa mama bikra maria na tusiwe watu wa kukaa na kuanza kusengenyana badala ya kutumia muda huo kumuomba mungu ili atusaidie katika mahitaji yetu mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku.
Aidha amewataka watu wenye tabia ya kujinufaisha kupitia shida za wengine kwa kujipatia mali na heshima kuacha vitendo hivyo badala yake wawe mstari wa mbele kuwasaidia wenye uhitaji.
Amesema kupitia mateso ya bwana yesu kristu msalabani inawapasa watu kubadilika na kuwa watetezi wa wajane,yatima na waliokatika shida mbalimbali na siyo kuwakandamiza bali wapewe faraja na upendo ili kama yalivyo mafundisho ya mungu.
"Wakati wa msiba watu wanajinufaisha kupitia mirathi ya marehemu watoto wanabaki wanahangaika,tuwe watetezi wao yatima,wajane na wengine wenye shida mbalimbali tusiwakandamize"amesema Askofu Sangu
Baadhi ya waumini wa Kanisa hilo Neema Chala mkazi wa Mtaa wa Ngokolo,amesema mafundisho hayo wakiyazingatia yatawawezesha kuwa katika msingi mzuri ikiwemo kuwasaidia watu wenye uhitaji na kulinda ndoa zao.
Muumini mwingine Paschal Juma amesema,Ibaada ya Ijumaa kuu inawakumbusha mateso ya bwana yesu kristu msalabani na kupitia mwezi wa kwaresma ambao wanaelekea kuuhitimisha umekuwa wa baraka kwao na wataendelea kuyafuata mafundisho yote.
0 Comments