Header Ads Widget

LOWASSA AFARIKI DUNIA

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.

Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango.

Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26,1953 na alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 na amefariki akiwa na miaka 71.

Post a Comment

0 Comments