Mkurugenzi mtendaji wa shirika la SEIDA Fredrick Ogenga akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha mradi wa vijana kilimo biashara utakaowanufaisha vijana na wanawake 25,000 wa mikoa miwili Shinyanga na Tabora
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
WAKULIMA 25,000 kutoka halmashauri nane za Mkoa wa Shinyanga na Tabora wanatarajia kunufaika na mradi wa Vijana kilimo biashara ambao utawasaidia katika kulima mazao ya biashara yanayostahimili ukame ambayo ni alizeti na mtama mweupe pamoja na mbogamboga kutokana na soko la mazao hayo kuwa la uhakika.
Akitambulisha rasmi mradi huo kwa wataalamu wa kilimo kutoka halmashauri nane mkurugenzi mtendaji wa shirika la SEIDA Fredrick Ogenga amesema mradi huo unaotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na
shirika la mpango wa chakula Duniani (WFP) utawanufaisha wakulima 25,000 kutoka halmashauri nane ambapo asilimia 70 ya wanufaika hao ni wanawake na asilimia 70 vijana.
Ogenga alisema wanufaika wa mradi huo watanufaika kwa miaka mitatu ambapo mradi huo umeanza Oktoba 2023 hadi Septemba 2026 ambapo mazao makuu ya mradi huo ni alizeti na mtama mweupe ikiwa ni pamoja na mbogamboga.
Mkurugenzi Ogenga alizitaja halmashauri ambazo zitanufaika na mradi huo kuwa ni Kishapu,Msalala, Shinyanga vijijini, Msalala, na Ushetu , kwa Mkoa wa Shinyanga, na kwa Mkoa wa Tabora ni Nzega, Igunga, Uyui, Sikonge, na Tabora Mji, ambao makundi maalumu yakiwemo ya watu wenye ulemavu watanufaika na mradi huo
Alisema malengo makubwa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza kipato cha vijana na wanawake katika mikoa ya Tabora na Shinyanga, ambapo kupitia mradi huo wazalishaji na wakulima wadogo watawezeshwa kuongeza kipato na kufanya uzalishaji wenye kukidhi na kufuata mahitaji ya soko, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa mbegu bora.
"Mbegu bora zitapatikana kupitia wazalishaji wa daraja la mbegu za kuazimia (QDS) kwenye kata na vijijini ili kupunguza upotevu wa mazao wakati na baada ya mavuno na pia kupitia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na mwisho kuimarisha vyama na asasi za wazalishaji, wakulima kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa masoko na huduma za pembejeo pia wanufaika hao watapatiwa vifaa vya kilimo "alisema Ogenga.
"Lengo la kwanza ni kuongezeka kwa ubora na uzalishaji wa mazao ya alizeti na mtama mweupe katika Mikoa ya Shinyanga na Tabora na hatimaye kuongeza kipato cha wakulima na makundi yanayolengwa,pia wakulima wadogo hasa wanawake na vijanana wataweza kupunguza changamoto ya upotevu wa mazao baada ya mavuno na kuongeza kipato cha kaya na jamii kuimarika kwa kujipatia ajira"aliongeza Ogenga .
Aidha alisema sifa za mkulima awe na umri wa miaka 18 na kuendelea, huku kipaumbele ni wanawake na vijana ambapo wanaweza kuchukua mtu zaidi ya mmoja kwenye kaya, vijiji na kata ambazo zina vikundi na vyama vya msingi wa mazao, mifuko ya kuweka na kukopa na makundi ya vijana na wanawake ambayo yametambuliwa na idara za mamlaka za halmashauri husika katika maeneo yanayolima mazao hayo.
"Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo upatikanaji wa mvua imekuwa siyo ya kutabirika na hivyo wakulima hasa wa kanda ya kati na maeneo mengine wamekuwa wakiathirika na kukosa mavuno, hivyo mazao haya yanavumilia hata kwa mvua chache, pia kutokana na changamoto ya mbegu watafundishwa wakulima ili waweze kutengeneza ili ziwe zinapatikana kwa urahisi"alisema Ogenga.
Alisema sababu nyingine kubwa ni soko la mtama mweupe kuwa la uhakika kwani Shirika la WFP linahudumia nchi ya Sudan Kusini kwa msaada wa chakula na mahitaji ya mtama mweupe ambayo ndiyo chakula kikuu cha nchi hiyo ambayo inahitaji zaidi ya tani 200,000 hivyo jambo la msingi ni kuhakikisha wakulima wanaongeza udhalishaji wa mtama huo, kwa kulima kilimo chenye tija.
Frank Lyimo ambaye ni meneja mradi kutoka kutoka SEIDA amesema mradi huo utaangalia mambo ya mavuno na upatikanaji wa ardhi na kuwawezesha kuwapatia kipato endelevu wakulima na kuhakikisha wanachukua takwimu ili kujua mabadiliko gani yamefanywa na wakulima hao.
".Pia tutaanzisha clabu za vijana kwa ajili ya kupima udongo kukodisha vifaa vya kilimo kutoa huduma kwa ajili ya wenzao na kuhakikisha asilimia tano wanakuww na uhakika wa chakula wakati wote wa mwaka, targeti yetu kwa mkoa wa Shinyanga ni kuwa na walengwa 10, 000 , ambapo Msalala tunatarajia kupata wakulima 4,631, Kidhapu 2,414, na Shinyanga 2,956, sawa na asilimia 40.amesema Lyimo
Katika Mkoa wa Tabora tunatarget wakulima 15,000 ambayo ni asilimia 60 ambapo Igunga 4,056, Nzega 5,096, Uyui 4,025, Skonge 1,824 hivyo ukiunganisha na wakulima wa Shinyanga wanakuwa 25,000 sawa na asilimia 100.
Afisa kilimo wa halmashauri ya Kishapu Sabinus Chaula amelishukuru shirika kwa kuleta mradi huo kwani utasaidia kuongeza chakula kimkoa hivyo utachochea wakulima kulima kilimo chenye tija na wananchi wataongeza kipato kutokana na kupatikana kwa soko la uhakika.
Naye afisa kilimo kutoka Shinyanga Edward Maduhu alisema mradi huo unaenda kubadilisha maisha ya wananchi wa Shinyanga hivyo wameufurahia sana sio kwamba walikuwa hawalimi walikuwa wakilima lakini walikuwa hawana soko la uhakika hivyo wataenda kuhamasisha vikundi na pia watahamasisha wakulima mmoja mmoja aweze kujikita kwenye kilimo bora cha mazao hayo ili aweze kuongeza kipato .
Afisa kilimo kutoka ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Ancila Karani mradi huo utasaidia halmashauri ambazo zimeingia kwenye mradi, kutokana na mvua za Shinyanga kuwa chache ambayo inaunguza mahindi, lakini kwa mtama na alizeti inatosha hivyo niwaombe wakulima waliolengwa na mkulima mmoja mmoja wachangamkie fursa hiyo.
"Tukiangalia takwimu za mwaka 2019/2020 mkoa wa Shinyanga ulipata tani 40,308, mwaka 2020/2021 ulipata tani 41530, na mwaka 2021/2022/ulipata tani 27,716, na mwaka 2022/2023 tani 25,091, hivyo niwaombe mwaka huu wa 2024 waongeze bidii kwa kilimo cha mtama mweupe na alizeti ili zipatikane tani nyingi zaidi kwa sababu soko la uhakika na lenye bei nzuri limepatikana,"amesema Ancila.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la SEIDA Fredrick Ogenga akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha mradi wa vijana kilimo biashara utakaowanufaisha vijana na wanawake 25,000 wa mikoa miwili Shinyanga na Tabora
Afisa kilimo kutoka Shinyanga Edward Maduhu akizungumza juu ya mradi wa kilimo kwamba utawanufaisha wakulima kwa kulima kimo chenye tija
Afisa kilimo wa halmashauri ya Kishapu Sabinus Chaula akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wananchi wake watafaidika na kilimo hicho kwa kulima mtama na alizeti hivyo watahamasisha ili wakulima waweze kujiongezea kipato
Afisa kilimo kutoka ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Ancila Karani amesema wananchi wahalmashauri zote zilizolengwa ni vizuri kuchsngamkia fursa ya kilimo cha pamba na alizeti ili kujiongezea kipato
Wataalamu wa kilimo wakiwa kwenye kikao cha kutambulishwa mradi wa vijana kilimo biashara utakaowalenga wananchi 25,000
Wataalamu wa kilimo wakiwa kwenye kikao cha kutambulishwa mradi wa vijana kilimo biashara utakaowalenga wananchi 25,000
Wataalamu wa kilimo wakiwa kwenye kikao cha kutambulishwa mradi wa vijana kilimo biashara utakaowalenga wananchi 25,000
Wataalamu wa kilimo wakiwa kwenye kikao cha kutambulishwa mradi wa vijana kilimo biashara utakaowalenga wananchi 25,000
Mtaalamu akifuatilia mradi wa kilimo cha mazao ya mtama mweupe nambogamboga
Wataalamu wa kilimo wakiwa kwenye kikao cha kutambulishwa mradi wa vijana kilimo biashara utakaowalenga wananchi 25,000
0 Comments