Kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi mkoa wa kikodi Kahama.
Na Kareny Masasy,Kahama
MKUU wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema kodi inamchango mkubwa kwa maendeleo na kasi kubwa ya ulipaji kodi ndiyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo baadhi ya wafanyabiashara waache kutisha wateja na kuendesha biashara za magendo.
Mhita amesema hayo jana tarehe 2/Desemba ,2023 alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha shukrani kwa mlipakodi mkoa wa kikodi Kahama huku akiwatunukiwa vyeti baadhi ya wafanyabishara wakubwa na wadogo kwa jitihada za ulipaji kodi kwa ufanisi.
Mhita amesema ulipaji kwa kodi kwa hiari unaonyesha jitihada za kuunga mkono serikali kufanikisha miradi ya maendeleo kama ujengaji wa miundombinu ya barabara,shule, hospitali nawapongeza TRA Kahama namna ya usimamizi mzuri wa ulipaji kodi.
Kauli mbiu “Kodi yetu maendeleo yetu tuwajibike” ili kuwa na kumbukumbu sahihi za baishara yako lazima ujue kodi inayotozwa hivyo utunze kumbukumbu na hapo utalipa vizuri kuliko usiotunza kumbukumbu”amesema Mhita.
Mhita amewakumbusha wafanyabiashara matumizi ya utumiaji wa mashine za kielektroniki (EFD) ikiwa lazima kuendana na matumzi ya kidijitali sambamba na muuzaji kutoa risiti kwa wateja na kuondoa dhana potofu ya kueleza wanaibiwa ambapo ushauri watumie risiti.
Naibu mkurugenzi wa fedha kutoka TRA makao makuu Anna Mdeme amesema Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele na kufanya mapinduzi makubwa ya usimamizi wa kodi kwa kutatua upungufu wa watumishi na kuridhia uboreshaji wa mamlaka hivyo wameimarika kwa kiasi kikubwa nakutambua mchango mkubwa wa walipa kodi.
"Mwaka wa fedha 2022/2023 mamlaka ilifanikiwa kukusanya sh Trioni 24.11 sawa na ufanisi wa asilimia 97.4 ya makusanyo ya jumla ya lengo na ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.2 ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2021/2022 hivyo wanashukuru walipa kodi kwa dhana ya kauli moja na walipa kodi”amesema Mdeme.
Ukusanyaji wa mapato ni shughuli endelevu inahitaji kuimarika siku zote Mwaka 2023/2024 kuanzia Julai mamlaka ina lengo la kukusanya sh tironi 28. 4 ikiwa Sh Trioni 27.8 Tanzania bara na Bilioni 520.6 Tanzania visiwani mafanikio yameridhisha mpaka sasa .
Mdeme amesema kuanzia mwaka 2022/2023 Julai hadi Septemba robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wamekusanya sh Trioni 6.58 sawa na ufanisi asilimia 97.53 makusanyo hayo ni ongezeko kubwa la asilimia 11.05 ila mwaka uliopita walikuwa na ongezeko la asilimia 8.
Mdeme amewashauri wafanyabiashara waache kuficha taarifa zao ili kuweza kukusanya mapato,hivyo huduma bora zenye uwajibikaji ndiyo msingi bora wa kulipa kodi na mmamlaka imeeleza kutoa elimu zaidi ili kuleta uwajibikaji kwa walipa kodi.
Kaimu meneja kutoka (TRA) mkoa wa kikodi Kahama Wisaka Kamwamu amesema mapindizi kwa ulipaji kodi umeleta ufanisi mkubwa kwa kila siku kwa wafanyabiashara na wafanyakazi.
“Ikiwa mkoa wa kikodi Kahama umefanikiwa kukusanya kodi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Julai hadi Novemba mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kukusanya sh Bilioni 6.59 sawa na ufanisi wa asilimia 125 ambapo malengo ya makusanyo yalikuwa ni sh Bilioni 7.2”amesema Kamwam.
Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabishara,viwanda na kilimo (TCCIA ) wilaya ya Kahama Charles Machali amesema kutunukiwa vyeti wafanyabiashara na kuongezeka mapato ni jitihada zilizofanywa kwa ushirikiano kwani zamani TRA ilikuwa adui sasa ni marafiki.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita katikati ni mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara,viwanda na kilimo Charles Machali wakimpongeza mkurugenzi wa shule za Anderleck na Rocken Hill akipokea cheti cha pongezi kutoka TRAMfanyabiashara akipongezwa kwa kupewa cheti cha ulipaji kodi kwa ufanisi kutoka TRA.
viongozi wa TRA akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita pamoja na mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara, viwanda na kilimo Charles Machali wakisubiri kutoa tuzo na vyeti
Kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi mkoa wa kikodi Kahama
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya kielele cha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi
Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara,viwanda na kilimo (TCCIA) wilaya ya Kahama Charles Machali akitoa neno la shukrani kwa TRA
0 Comments