Header Ads Widget

WAFANYAKAZI BENKI YA CRDB KANDA YA MAGHARIBI WAFANYA SHEREHE

Meneja Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Benjamin Ngayiwa akifungua sherehe ya wafanyakazi wa benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga 

Na Amos John Shinyanga

Wafanyakazi wa benk ya CRDB kutoka matawi ya Mbogwe,Kahama,Tinde ,Maganzo na Shinyanga wamekutana pamoja katika ukumbi wa Shypark Hotel mjini Shinyanga kwa lengo la kusherehekea na kudumisha umoja na mshikamano baina ya wafanyakazi wa benki hiyo.

Akifungua Sherehe hiyo Meneja Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Benjamin Ngayiwa amesema lengo la kukutana pamoja katika ukumbi huo ni kutaka kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kudumisha umoja na mshikamano baina ya wafanya kazi wanaofanya kazi na benki hiyo mkoa wa Shinyanga.

Aidha Ngayiwa ameeleza kuwa kufanyika kwa aherehe hiyo ni pamoja na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB makao makuu Godfrey Butasingwa kuwataka Mamenwja rasilimali watu kuandaa sherehe itakayo wakutanisha wafanyakazi wa benki hiyo na kufurahi pamoja.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amewataka wafanyakazi wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga kufurahia kwa pamoja huku wakitafakari namna watakavyoendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi wao ili kanda ya Magharibi iendelee kufanya vizuri katika kanda zote za CRDB Nchini.

Costansia Albinus ni meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Maganzo wilaya ya Kishapu na Erick Chambwenenge meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama wameushukuru uongozi wa Kanda kwa kuandaa Sherehe hiyo maana kufanyika kwa sherehe hiyo kutakuwa ni chachu ya kuchochea Benki ya CRDB kufanya vizuri katika matawi yao na Kanda kwa ujumla.

Sherehe hiyo imejumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa bao,mchezo wa Draft ,mchezo wa karata ,mchezo wa rede kwa wanawake na michezo mingine ambapo washindi wa michezo hiyo wameondoka na zawadi mbalimbali .

Meneja Rasilimali watu kutoka Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Benjamin Ngayiwa akifungua sherehe ya wafanyakazi wa benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiendelea kupata burudani.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakijiandaa kwa ajili ya kuanza michezo.
Luther Mneney Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Shinyanga akifanya utambulisho wa wafanyakazi wa Tawi hilo.

Costansia Albinus meneja wa benki ya CRDB Tawi la Maganzo akifanya utambulisho wa wafanyakazi wa Tawi hilo.

Post a Comment

0 Comments