Header Ads Widget

TRA YATOA ELIMU YA MLIPAKODI KWA CHAVITA KAHAMA

 TRA YATOA ELIMU YA MLIPAKODI KWA CHAVITA KAHAMA

Na kareny Masasy.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama imetoa elimu  kwa  watu wenye walemavu  wa kutosikia  (viziwi )namna ya kuwa wazalendo katika  ulipaji wa kodi  kwa mujibu wa sheria  na taratibu zilizowekwa.

Ofisa Mawasiliano  na elimu kwa mlipa kodi  kutoka mamlaka  hiyo  Aniceth Ndailagije amesema  hayo  jana wakati akitoa mafunzo ya siku moja kwenye chama Cha  viziwi Tanzania (chavita) kwa wilaya ya Kahama inayojumuisha halmashauri tatu za Msalala,Ushetu na manispaa Kahama.

" Tunaomba elimu hii mmeipata mkatoe ushirikiano  na  muwe mabalozi wazuri kwa wengine  kwa kuzifahamu   sheria na kanuni zake ikiwa kila mwaka wa fedha  Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imeenda ikiziboresha zaidi na mzisome au kuomba ufafanuzi kwenye mamlaka husika" amesema Ndailagije.

Ndailagije amesema  kupitia kundi hili na chama chenu  mnayo fursa ya kuiwezesha serikali kupata mapato yake stahiki na hatimaye kutoa huduma bora  zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi.Ndailagije amesema  watii  wajibu  wa kulipa kodi  kwani taifa lolote ikiwemo Tanzania  linaendeshwa  kwa shughuli  za fedha zitokanazo na kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Ndailagije  amesema elimu iliyotolewa waizingatie kwani  itawajengea uwezo wao wa kusikia kulipa kodi kwa wakati pamoja na kutatua changamoto zao wanazo kutananazo katika mazingira ya biashara.Zawadi masoudi mwenyekiti wa chama chavita  Wilaya ya Kahama  amesema waliiomba mamlaka hiyo kuwapatia elimu ya mlipa kodi  na TRA imewaona  na kuwaletea mafunzo ili waifahamu Sheria zilizopo.

"Tunaipongeza mamlaka  hii  tumejifunza vitu ambavyo hatukuvijua ikiwa  baadhi yetu ni wafanyabiashara  watakuwa wamenufaika"amesema Zawadi.

 Maafisa wengine wa  TRA  walibainisha kuwa madhumuni ya kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu hasa viziwi ni kuwapatia elimu ya mlipa kodi na kuweza kuwajibika kama sheria za kodi zinazoelekeza kwa kila mtu bila ubaguzi.



Mafunzo ya elimu ya mlipa kodi yakiendelea kwa walemavu wasiosikia.


Washiriki wakiendelea na mafunzo ya elimu ya mlipa kodi.

Post a Comment

0 Comments