Header Ads Widget

VIONGOZI WA SENET SHINYANGA WAZINDUA TAWI JIPYA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA HOMBOLO TAWI LA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

VIONGOZI wa Senet ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Shinyanga wa umoja wa vijana (UVCCM),wamezindua Tawi jipya la Senet katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga, pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi wa Senet hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika jana chuoni hapo huku Mgeni Rasmi akiwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Rafael Nyandi.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan, amesema baada ya kuzinduliwa tawi hilo watakuwa wamefikisha matawi 13 ya Senet vyuoni, huku akiwasihi wanachuo wajiunge na Senet ili wapate kunufaika na matunda ya nchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mwanachuo ukiwa ndani ya Senet unakuwa upo salama, hivyo nawasihi vijana jiungeni kwa wingi,”amesema Sultan.
Naye Katibu ya UVCCM Mkoa wa Shinyanga Rafael Nyandi, amewasihi wanachuo hao wawe Raia wema, na watakapo hitimu masomo yao waje kuwa Watendaji wazuri na kumsaidia Rais Samia kuchochea maendeleo ya taifa, pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Aidha, Katibu wa Senet Mkoa wa Shinyanga Masunga Mazoya alitangaza viongozi wa Senet ambao wameshinda kwenye uchaguzi wa Senet katika Chuo hicho cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga, kuwa Hadija Abdala ameshinda nafasi ya Uenyekiti, Katibu ni Eddy Makoye, Hamasa Anita Ntui.
Ametangaza nafasi za mbili za wajumbe, kwamba walioshinda ni Frank Chimika na Stanley Rashidi.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Rafael Nyandi akizungumza kwenye uzinduzi wa Tawi la Senet na uchaguzi wa Viongozi katika Chuo Cha Hombolo Tawi la Shinyanga.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan akizungumza kwenye uzinduzi wa Tawi la Senet na uchaguzi wa viongozi katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga.
Katibu wa Senet Mkoa wa Shinyanga Masunga Mazoya akitangaza Matokeo ya viongozi wa Senet Tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Tawi la Senet na uchaguzi wa viongozi katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga.
Hadija Abdala ambaye alishinda nafasi ya Uenyekiti wa Senet Tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga.
Washindi wengine wa nafasi mbalimbali ya uongozi katika Senet ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga.
Wanachuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa Tawi la Senet na uchaguzi wa viongozi wao.

Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Chuo cha Hombolo Tawi la Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments