Header Ads Widget

JKT-TANZANIA YATAMBA KUTOA KICHAPO CHA DOUBLE K, KWA KAGERA SUGAR UWANJA WA CCM KAMBARAGE SHINYANGA

JKT-TANZANIA YATAMBA KUTOA KICHAPO CHA DOUBLE K, KWA KAGERA SUGAR UWANJA WA CCM KAMBARAGE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TIMU ya Mpira wa Miguu JKT-Tanzania ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara NBC, imetamba kuichakaza Timu ya Kagera Sugar kichapo cha Kizalendo maarufu ‘Double K’ katika mchezo wao siku ya ijumaa.

Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Timu ya JKT-Tanzania Masau Bwire, amebainisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Timu ya JKT-Tanzania Masau Bwire.

Amesema Timu hiyo imeuchagua Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kama Uwanja wao wa nyumbani katika msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya uwanja wao wa nyumbani wa Meja Generali kufanyiwa ukarabati mkubwa, huku akitamba kuwa katika Uwanja huo Shinyanga kila atakaye cheza naye lazima achezee kichapo cha Double K.

“Tunatoa wito kwa Mashabiki wa JKT-Tanzania wasikate tamaa katika Michezo yetu miwili iliyopita ambayo tulipoteza dhidi ya Yanga na KMC ambapo tulikuwa hatajajipanga vizuri kutokana na Maandalizi ya Mechi zetu za Kitaifa za JKT Prince, lakini kwa sasa tupo vizuri,”amesema Masau.

Aidha, amesema wachezaji wao wako vizuri kiafya na hakuna majeruhi na kikosi cha kipo bora na wamejipanga kufanya vyema katika mechi zao zote zijazo na watamaliza msimu wa ligi kuu katika nafasi nzuri.

Ametoa wito kwa wakazi wa Shinyanga wawaunge Mkono kama Timu yao ya nyumbani, na wajitokeze kwa wingi kuwashangilia ili kuwapatia nguvu katika michezo yao na kupata ushindi.

Amesema katika Mchezo wa huo wa siku ya ijumaa Mageti yatakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi, na kiingilio mzunguko itakuwa Sh.2,000 na Jukwaa Kuu Sh.3,000 na kwamba kwa wale ambao siyo na kadi ya mtandao (N-Card) watakwenda na Sh,1,000 ili kukatiwa kadi hiyo.

Post a Comment

0 Comments