Header Ads Widget

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTENGA MUDA WA KUZUNGUMZA NA WATOTO WAO


Ma Mchungaji  Baraka Laizer wa Kanisa la Philadelfia Miracle Temple Evaline Msangi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto kwenye sherehe yao

Suzy Luhende, Shinyanga Press

Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kumpendeza Mungu, kuwahimiza kwenda kanisani kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu, pamoja na kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao, ili wasijiingize kwenye vitendo visivyompendeza Mungu


Agizo hilo limetolewa na mama mchungaji wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple
Evaline Msangi
lililopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kwenye sherehe ya watoto iliyofanyika kanisani hapo, ambapo amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kwenda kanisani kujifunza neno la Mungu.

Evaline amesema wazazi wengi wamekuwa hawatengi muda wa kuzungumza na watoto wao kwani wanakuwa wapo bize na shughuli zao na hawawahimizi watoto kwenda kanisani kujifunza neno la Mungu, hivyo amewaomba wahamasishe watoto wapende ibada ili baadae waweze kuwa na kizazi kinachomjua Mungu.

"Niwaombe wazazi tuwaombee watoto wetu ili wasijiingize kwenye vitendo visivyo na maadili mema, na tuwalee katika maadili mema ya kumpendeza Mungu katika siku zote za maisha yao wamjue Mungu na kumtumikia, hivyo tusiwaache watoto nyumbani wakajifunza mambo ya mitaani ambayo wewe mzazi huyapendi utajisikia vibaya "amesema Evaline.

"Tuwafundishe neno la Mungu watoto wetu ili baadae tuweze kuwa na furaha, ni kweli tunakimbizana na maisha ili kuweza kujipatia chochote lakini tukumbuke kuweka muda wa kuzingumza na watoto wetu,pia niwapongeza walimu wanaofundisha watoto na ninawashukuru watoto wote waliohudumu katika wiki lote la watoto kwani mmefanya vizuri na Mungu aendelee kuwatumia mkaendelee kufanya mambo makubwa zaidi"amesema Evaline
.

Kwa upande wake mchungaji Anania Clementi amewapongeza watoto kwa huduma wslioifanya katika sherehe yao hivyo amewaomba waendelee kumtumikia Mungu kwa nguvu zote ili baadae wakawe watumishi wazuri.

Mmoja wa watoto hao Dainess Ditrick amesema anamshukuru Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Baraka Laizer kwa kuendelea kuwalea vizuri na kuwafundisha neno la Mungu, hivyo ameomba kwaya ya watoto iendelee kuhudumu siku za ibada kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kukuza vipaji vya uimbaji kwa watoto 

Aidha Mwalimu Dionisio Kaijage ambaye ni mwenyekiti wa Chama Cha wanawake wa kanisa hilo amewapongeza watoto kwa kufanya huduma nzuri kanisani ya uimbaji, kuhubiri na kufanya huduma zingine mbalimbali, ambapo aliguswa kutoa zawadi kwa watoto wote wa kanisa hilo

Mwalimu wa watoto wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Neema Fredrick akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto

Ma Mchungaji wa Kanisa la Philadelfia Miracle Temple Evaline Msangi akizungumza na kuwasihi watoto waishi katika maadili mema ya kumpendeza Mungu
Mwalimu wa watoto wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Neema Fredrick akizungumza na kuwaomba wazazi wawaruhusu watoto kwenda kanisani ili kujifunza yaliyo mema
Ma Mchungaji wa Kanisa la Philadelfia Miracle Temple Evaline Msangi akipokea zawadi kwa watoto kwa niaba ya mchungaji Baraka

Ma Mchungaji wa Kanisa la Philadelfia Miracle Temple Evaline Msangi akiwapongeza watoto kwa kufanya vizuri sherehe yao

Mchungaji Anania Clement akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto

Mchungaji Anania  Clementi akipokea zawadi kutoka kwa watoto kwa shukrani ya kuwafundisha neno la Mungu na kuwajenga katika maadili mema

Mwalimu wa watoto wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Neema   
Fredrick  akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto
Walimu wa watoto wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto
Mwalimu Dionisio Kaijage akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto


Mwalimu Dionisio Kaijage akiwapa zawadi watoto kwa kuwapongeza kuhudumu vizuri

Watoto wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mwalimu Dionisio Kaijage akiwapongeza watoto kwa kufanya huduma mbalimbali kanisani
Watoto wakiingia kanisani kwa ajili ya kuanza ibada
Watoto wakiimba kanisani


Watoto wakiingia kanisani kwa ajili ya kuanza ibada
Wazee wa kanisa katika siku ya watoto
Watoto wakisikiliza neno siku ya sherehe yao
Watoto wakisikiliza neno siku ya sherehe yao
Wazee wa kanisa katika siku ya watoto

Watoto wakisikiliza neno siku ya sherehe yao
Watoto wakisikiliza neno siku ya sherehe yao
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakisikiliza neno la Mungu kutoka kwa watoto






Post a Comment

0 Comments