Header Ads Widget

BENKI YA CRDB YAINGIA MAKUBALIANO NA KLABU YA YANGA KUSAIDIA USAJILI WA WANACHAMA NA MASHABIKI

  

Benki ya CRDB imeingia mkataba wa makubaliano na Yanga kutoa kadi kwa wanachama wa klabu Yanga katika kuongeza ufanisi wa usajili na masuluhisho ya kifedha.

Akizungumza wakati hafla kusaini makubaliano hayo iliyofanyika Julai 1, 2023, Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Boma Raballa amesema kadi hizo zitawawezesha mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania bara kujisajili na kulipia michango yao ya uanachama kupitia mtandao wa matawi zaidi ya 240 wa Benki ya CRDB.
“Kupitia kadi hizi zilizopewa jina la TemboCard Young Africans wanachama wa klabu hii wataweza kufanya miamala kupitia mashine za kutoa fedha (ATMs) hadi milioni 2, kufanya manunuzi kupitia mashine za malipo (PoS), pamoja na malipo ya mtandaoni (online payment) hadi milioni 20,” alisema Raballa huku akibainisha kuwa wanachama hao pia wataunganishwa na mifumo ya kidijitali ya SimBanking na Internet banking.

Raballa pia alianisha kuwa kupitia kadi hizo za TemboCard Young Africans wanachama na washabiki wa klabu hiyo pia watapata bima ambayo inatoa mkono wa pole wa Shilingi milioni 3 pindi mwanachama anapofariki ya milioni 3, Shilingi milioni 2.5 anapofiwa na mume au mke, na Shilingi milioni 2 endapo atapata ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wake Rais wa Yanga, Injinia Hersi Saidi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kufungua milango ya ushirikiano na klabu hiyo itakayosaidia kuongeza ufanisi katika usajili. Injinia Hersi alisema ukubwa Benki hiyo yenye mtandao mpana ndani na nje ya nchi utakwenda kusaidia kuongeza kasi ya usajili wa wananchama wengi zaidi kulinganisha na sasa hivi.

“Mchakato wetu wa usajili wa wanachama umekuwa na mafanikio makubwa sana ukitufanya kuwa klabu inayoongoza kwa Idadi ya wananchama katika ukanda huu wa jangwa la sahara, lakini ni ukweli usiopingika kuwa bado hatujafikia lengo kwani matawi yetu mengi yamekosa miundo mbinu sahihi. Ni imani yetu ushirikiano huu na Benki ya CRDB utakwenda kuongeza kasi ya usajili,” aliongezea Injinia Hersi.
Akizungumzia kuhusu zoezi usajili wa wananchama kupitia Benki ya CRDB, Injinia Hersi alisema kuanzia tarehe 5 Julai 2023 wanachama wa klabu hiyo wanaweza kufanya usajili katika matawi yote ya benki hiyo yaliyosambaa kote nchini bila gharama yoyote.

Post a Comment

0 Comments