Dkt. Martha Jotham akitoa neno fupi kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Buzwagi na kuwatia moyo wa kuendelea kupenda kazi yao.
Mhandisi Zonnastraal Mumbi (PEng), akiongea akifungua hafla hiyo ya wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Zonnastraal Mumbi (P Eng) Akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wafanyakazi katika hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
***
Wanawake  nchini wametakiwa kujitokeza kuchangamkia fursa za kufanya kazi migodini badala ya kuamini kuwa kazi za migodini na sekta ya madini kwa ujumla ni za wanaume.
Wito huo umetolewa wakati wa  hafla ya  usiku wa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Barrick Buzwagi, uliopo Kahama mkoani Shinyanga ambapo upo katika mchakato wa kufungwa.
Akifungua  hafla hiyo,Mwakilishi wa Meneja Mkuu  wa mgodi wa Barrick Buzwagi,Mhandisi Zonnastraal Mumbi (PEng), alisema hafla hiyo ni ya kusherehekea na  kuwapongeza wanawake wote wanaofanya kazi katika mgodi huo na kuwatia moyo wa kuendelea kujiamini zaidi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Dkt. Martha Jotham, ambaye ni Mtawala na Mkufunzi wa Taasisi ya Biblia duniani (WIBI)  ya Mkoani wa Mwanza, aliwataka wanawake nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini na alipongeza jitihada zinazofanywa na Mgodi wa Buzwagi kwa kutambua mchango wa wanawake katika mgodi .
Dkt, Jotham alitoa rai kwa Wanawake hao  kutambua kuwa wao ni wa thamani na  wa pekee pamoja na kuwa wanafanya kazi ngumu na wanakutana na changamoto nyingi wanatakiwa kujiamini kwa kile wanacho kifanya ndiyo maana mgodi unatambua jitihada zao katika utendaji kazi wao na ndiyo maana wameandaliwa hafla hii.
Aliwashauri kuwa mambo ya msingi wanayopaswa kuyazingatia  wanapokuwa  kazini ni kujitambua kwa kuchapa kazi kwa bidii, kujipenda kwa kuhakikisha wanavaa vizuri na kula vizuri na kujiwekea akiba kutokana na kipato  chao kwa ajili ya kuwasaidia katika siku za mbele.
Dkt. Jotham, aliwataka kumtanguliza Mungu mbele katika kazi zao, kujiamini na kuthubutu wa  kutenda mipango ya maendeleo ya jamii waweke mikakati na mipango yao vizuri wakitabua maisha yao hayahitaji mtu mwingine,maisha yao yanawahitaji wao.
Katika hafla hiyo pia wanawake wa mgodi huo walizawadiwa zawadi mbalimbali.







 
 
       
 
 
