Header Ads Widget

SHIRIKA LA TCRS LATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WANAOTOKA KWENYE FAMILIA ZENYE MAZINGIRA MAGUMU WILAYANI KISHAPU

SHIRIKA LA TCRS LATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WANAOTOKA KWENYE FAMILIA ZENYE MAZINGIRA MAGUMU WILAYANI KISHAPU.

Shirika lisilo la Kiserikali linalojulikana kwa jina Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) limetoa msaada wa taulo za kike (reusable) kwa wanafunzi wakike 315 wa Shule za Sekondari Bulekela Kata ya Masanga na Isoso kata ya Kishapu Wilayani Kishapu wanaotoka kwenye familia zenye uwezo mdogo kiuchumi pamoja na wenye ulemavu.
Msaada huo umetolewa sambamba na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa shule hizo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Hedhi Dunuani yenye kauli mbiu isemayo “WANAWAKE NA WASICHANA WOTE WANAPASWA KUWA NA UWEZO WA KUSIMAMIA HEDHI YAO KWA HESHIMA NA UTU.” Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wakike wanaweza kukabiliana na vishawishi vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo na kupoteza ndoto zao za maisha yao.
Akizungumza wakati wa tukio hilo lililowashirikisha watumishi wa sekta ya Afya ofisi ya DMO Wilaya ya Kishapu kwa kufadhiliwa na shirika la kimataifa la Finish Evangelical Lutheran Mission (Felm) kwa fedha kutoka serikali ya Finland; mwakilishi wa msimamizi wa mradi wa TCRS Kishapu Bwana Emmanuel Samwel amesema malengo ya kutoa msaada wa taulo za kike na kuwaelimisha wanafunzi kuhusu afya ya uzazi ikiweno HEDHI salama ni kuihamasisha jamii kuona kuwa Hedhi sio kitu cha ajabu bali ni jambo la kawaida linalopaswa kuchukuliwa kwa uzito katika familia ili kumlinda mtoto wa kike.
Emmanule Samweli mwakilishi wa msimamizi wa mradi TCRS Kishapu.

Aidha, ametoa wito kwa kinababa (Wanaume) kuwasapoti watoto wao wa kike kwa kuwanunulia Pedi na mahitaji mengine na kulichukulia swala hilo kwa uzito mkubwa ili kumkomboa mtoto wakike katika dimbwi la vishawishi vinavyoweza kumpotezea ndoto zake za mfanikio.
Akieleza mafanikio ya Shirika la TCRS Emmanuel Samwel, amesema Shirika linaendelea kufanya shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii ikiwemo kujenga vyoo vya kisasa mashuleni na kuweka vyumba maalum vya wanafunzi wakike kubadilishia kwa malengo ya kuisapoti serikali katika kumlinda mtoto wa kike.
Mwalimu mlezi wa Shule ya Sekondari Bulekela, Mwalimu Siku Mwinuka amesema awali kabla Shirika la TCRS kutoa msaada wa Pedi kwa wanafunzi wa kike kulokuwepo na changamoto ya baadhi ya wanafunzi hao kukatisha masomo kwa takriban siku tatu hadi siku sita kila mwezi wakiwa katika kipindi cha hedhi kutokana na familia zao kuwa na uwezo mdogo kiuchumi na kushindwa kukidhi mahitaji ya mtoto wa kike kujikinga na hali hiyo huku akilishukuru shirika la TCRS kuja na mpango huo ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia wanafunzi wakike kufaulu masomo yao.
Baadhi ya wanafunzi waliopata msaada huo wamelishukuru shirika la TCRS na FELM kuwakumbuka huku wakieleza kuwa baada ya kupatiwa taulo za kike wataweza kufanya bidi katika masomo yao na kufaulu kwakuwa changamoto iliyokuwa inasababisha washindwe kufanya vizuri imetatuliwa ambapo wamesema walikuwa wanalazimika kutoroka masomo wakati wa kipindi cha Hedhi kutokana na kukosa pedi.
Mwanafunzi Leah Simon wa shule ya Sekondari Bulekela wilayani Kishapu.

Rehema Jumanne ni Mratibu wa Afya ya uzazi, Mama na Mtoto ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya Kishapu amesema ili Hedhi iwe salama ni lazima kuwepo na namna ambayo upatikanaji wa taulo za kike unakuwa ni wa uhakika ili kuwawezesha watoto wakike kujisitiri wakati wa hedhi lakini jambo la msingi Zaidi ni elimu ya matumizi sahihi na utunzaji yanayoenda sambamba na usafi wa mwili hususani wakati wa siku za hedhi.
Rehema Jumanne Mratibu wa Afya ya uzazi, Mama na Mtoto ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya Kishapu.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kishapu Bi. Mwajuma Abed amewafundisha mabinti hao somo la ukatili wakijinsia na kuwataka kujilinda na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao ikiwa ni pamoja na kupata mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya ngono.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kishapu Bi. Mwajuma Abed akifundisha wanafunzi soma la ukatili wa kijinsia.


Post a Comment

0 Comments