Header Ads Widget

TAASISI YA FLAVIANA YAKABIDHI MATUNDU YA VYOO 24 SHULE YA SEKONDARI MAZINGE, NA CHUMBA MAALUMU CHA KUJISTILI HEDHI

Taasisi ya Flaviana yakabidhi matundu vya vyoo 24 shule ya Sekondari Mazinge na chumba maalumu cha kujistili hedhi.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TAASISI ya Flaviana Foundation imekabidhi matundu ya vyoo 24 na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga, na kuwaondolea adha wanafunzi kujisaidia kwa Foleni.

Makabidhiano hayo ya matundu ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi yamefanyika leo Juni 1,2023 katika Shule hiyo ya Sekondari Mazinge, huku Mgeni Rasmi akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata, akizungumza wakati wa kukabidhi matundu hayo vyoo, amesema aliguswa na shule hiyo ya Sekondari Mazinge kukabiliwa na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo, na kulazimika wanafunzi kujisaidia kwa foleni, huku watoto wa kike wakiwa hawana chumba maalumu cha kujistili na hedhi.

“Nawaomba wanafunzi miundombinu hii ya vyoo muitunze na muwe wasafi, na msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu, na wanafunzi wa kike msiwe watoro shuleni sababu ya kuwa katika siku zenu, vyumba vya kujistili na hedhi tumewajenga katika vyoo hivi ambavyo tumekabidhi leo,”amesema Flaviana.

Naye Meneja Miradi kutoka Taasisi hiyo ya Flaviana Foundation Lineth Masala, amesema ujenzi huo wa mtundu ya vyoo 24 katika Shule hiyo ya Sekondari Mazinge, ulianza Rasmi March Mwaka huu na kukamilika june kwa gharama ya Sh.milioni 58 kupitia ufadhili wa Diamonds do Good.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, ameipongeza Taasisi hiyo ya Flaviana Foundation kwa kuiunga Mkono Serikali kutatua matatizo mbalimbali katika Sekta ya Elimu, na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano, huku akiwataka wanafunzi wavitumie vyoo hivyo kwa matumizi sahihi na siyo kuharibu miundombinu yake.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba, amesema awali shule hiyo walikuwa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa mtundu ya vyoo, ambapo walikuwa na matundu Sita, matundu Manne (4)yanatumiwa na wanafunzi wa kike 507, na mawili (2) wanafunzi wa kiume 494, hivyo kupata matundu hayo 24 yatapunguza upungufu uliokuwepo awali na shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,001

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo akiwamo Mary Maximilian, amesema upatikanaji wa mtundu hayo ya vyoo 24, ambayo 12 ya wanafunzi wa kike, na 12 kiume, yatawasaidia kuondokana na usumbufu wa kujisaidia kwa foleni, pamoja na kupata vyumba maalumu vya kujistili na hedhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.

Mkurugenzi wa Flaviana Foundation, Flaviana Matata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari ya Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 vya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba akisoma taarifa ya shule hiyo kwenye hafla ya kukabidhiwa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
Mwanafunzi Mary Maximilian akitoa shukrani ya kujengewa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata akiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 ya vyoo na chumba  maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Maofisa kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi matundu 24 vya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari ya Mazinge Manispaa ya Shinyanga.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akikata utepe kuzindua matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizindua matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akikata utepe kuzindua choo cha wasichana chenye matundu 12 pamoja na chumba maalumu cha kujistili hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge , kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akikata utepe kuzindua choo cha wavulana katika Shule ya Sekondari Mazinge, kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiangalia chumba ambacho kitakuwa kikitumiwa na wanafunzi wenye ulemavu kujisaidia.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Foundation, Flaviana Matata akifungua bomba la maji katika vyooo hivyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, akiwa na Flaviana Matata wakifungua mabomba ya maji katika vyoo hivyo.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akinawa mikono katika mabomba ya vyoo hivyo.
Muonekano wa choo cha wasichana ambacho pia kina chumba maalumu kwa ajili ya kujistili hedhi.
Muonekano wa choo cha wavulana.
Mkuu wa wiaya ya Shinyanga Johari Samizi (katikati) akiwa na Flaviana Matata wakiteta jambo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (katikati) awali akiwasili katika hafla ya kukabidhiwa matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha kujistili hedhi kutoka Taasisi ya Flaviana Matata.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (katikati) akiwa na Flaviana Matata (kulia) na kushoto ni Meneja Miradi kutoka Taasisi ya Flaviana Foundation Lineth Masala wakiteta jambo.
Picha za pamoja zikipigwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Flaviana Matata.
Picha za pamoja zikipigwa.
Viongozi wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi.
Flaviana Matata akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge.
Flaviana Matata akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge.
Awali Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi na Flaviana Matata wakielekea kuzindua matundu 24 ya vyoo na chumba maalumu cha hedhi katika Shule ya Sekondari Mazinge.

Post a Comment

0 Comments